Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia: Polisi jipangeni kwa uchaguzi 2024, 2025
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia: Polisi jipangeni kwa uchaguzi 2024, 2025

Spread the love

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amelitaka Jeshi la Polisi nchini kujipanga katika kuhakikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025, zinafanyika kwa amani bila kuigawa nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi, leo tarehe 4 Septemba 2023, jijini Dar es Salaam, Rais Samia amesema Serikali yake inakwenda kulitafutia fedha kiasi cha Sh. 125 bilioni, ili kuliwezesha kutekeleza majukumu  yake katika kipindi hicho.

“Mwakani tuna uchaguzi wa Serikali za Mitaa, nataka jeshi liwe makini kwelikweli huko katika maeneo mbalimbali, kusimamia haki itendeke, kusimamia usalama katika chaguzi zile, kuhakikisha zinakwenda kwa njia ya usalama,”

“ IGP nimemwambia hilo akaniletea bajeti ya karibu Sh. 125 bilioni ambayo nakwenda kuipekua na ikiwezekana niipate yote ili zile changamoto ziondoke muweze kufanya kazi zenu vizuri,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema ulinzi na usalama wa Tanzania unalitegemea Jeshi la Polisi “nasema kila siku Tanzania yetu ni moja tu hakuna tena Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulimwenguni, tukiweka vizuri ni sisi watanzania, tukiipasua pasua ni sisi watanzania.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!