Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Jeshi la Polisi laanzisha mifumo 13 kudhibiti upotevu wa majalada
Habari Mchanganyiko

Jeshi la Polisi laanzisha mifumo 13 kudhibiti upotevu wa majalada

IGP, Camilius Wambura
Spread the love

JESHI la Polisi kupitia kitengo chake cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), limeanzisha mifumo 13 ikiwemo mfumo wa kudhibiti upotevu wa taarifa na majalada. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 4 Septemba 2023 na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillius Wambura, katika hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa waandamizi wa jeshi hilo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi, amesema uanzishwaji wa mifumo hiyo ni kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan, lililotaka watumie TEHAMA katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuleta uwazi na ufanisi katika utendaji wao.

“Jeshi limefanikiwa kutengeneza mfumo wa mawasiliano ya ndani kuhusu kazi za kiofisi, ambao tumeanza kuutumia. Mfumo unarahisisha kazi na kuepuka matumizi ya karatasi, unatoa tafisiri ya wazi na mipaka ya majukumu na fursa, kupunguza gharama za uendeshaji, kupunguza upotevuw a taarifa na majalada pamoja na kwuezesha ofisi kufanya kazi kwa saa 24 kote duniani,” amesema IGP Wambura.

IGP Wambura ametaja mifumo mingine kuwa ni, mfumo wa kutoa taarifa za mali zilizopotea, mfumo wa rasilimali watu, mfumo wa usimamizi usalama barabarani, mfumo wa ujumbe mfupi, mfumo wa taarifa za wasafiri wanaoingia na kutoka kupitia mipaka ya nchi na mfumo wa usimamizi silaha za kiraia.

Mifumo mingine ni, mfumo wa usajili wanafunzi wa vyuo vya polisi, mfumo wa tuzo na tozo kwa ajili ya kukusanya na kuratibu maduhuli ya Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!