
RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Alhamis, tarehe 14 Oktoba 2021, amewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kuanzia ziara ya siku tatu mkoani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).
Amewasili akitokea Chato, mkoani Kilimanjaro alikoshiriki shughuli ya kilele cha Mbio za Mwenge Maalum wa Uhuru, Kumbukizi ya miaka 22 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Wiki ya Vijana.
Mara baada ya kumaliza shughuli hiyo, aliondoka kwenda Kilimanjaro ambapo kwenye uwanja wa ndege, amepokewa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo akiwemo Mkuu wa Mkoa, Stephen Kagaigai.
Akiwa mkoani humo, atafanya ziara na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Barabara ya Bomang’ombe-Sanya Juu-Kamwanga yenye kilomita 98.
More Stories
Rais Samia amteua Mkuu mpya wa majeshi
Kesi ya kina Mdee kusikilizwa siku 14 mfululizo
Dk. Tulia awataka Watanzania kuachana na imani potovu kuhusu sensa