Saturday , 4 February 2023
Home Kitengo Michezo Mugalu , Mhilu kuwakosa wa Botswana
Michezo

Mugalu , Mhilu kuwakosa wa Botswana

Chris Mugalu, mshambuliaji wa klabu ya Simba
Spread the love

 

Washambuliaji wawili wa klabu ya soka ya Simba Chriss Mugalu na Yussuf Mhilu wanatarajiwa kuikosa Mechi Kati ya Simba na Jwaneg Galaxy Fc ya Botiswana 17 Oktoba 2021 kutokana na Mugalu kusumbuliwa na majeruhi huku Mhilu jina lake lilichelewa katika usajiri wa klabu bigwa hivyo ataukosa pia mchezo wa marudiano 24 Oktoba 2021 hapa nyumbani. Anaripoti Damas Ndelema Tudarco (endelea)

Akizungumza kuelekea mchezo huo kocha wa timu hiyo Didier Gomes amesema kuwa kikosi chake kipo imara kwa ajili ya kwenda kupambana ugenini na kupata ushindi ila itawakosa wachezaji wake Yusuf Mhilu na Chriss Mugalu, ambapo Mugalu hajafanya mazoezi na wenzie kwani anasumbuliwa na majeraha huku pia Mhilu yeye jina lake lilichelewa katika usajili wa michuano hiyo ya Klabu Bingwa Barani Afrika hivyo atakosa michezo yote ya raundi hii.

“Mugalu ajafanya mazoezi na wenzie kwa pamoja kwani aliumia toka tunajiandaa na mchezo dhidi ya Biashara United lakini tulimchezesha dhidi ya Dodoma jiji akajitonesha na Mhilu yeye jina lake lilichelewa katika usajili wa michuano hiyo ya Klabu Bingwa Barani Afrika” alisema Gomes

Aidha klabu hiyo inataraji kuondoka Nchini leo kuelekea Botswana kwa ndege ya kukodi Ili kukabiliana na wapinzani wake hao.

Aidha kama Simba atashidwa kufuzu katika hatua hii basi ataangukia katika michuano ya kombe la shirikikisho Barani Afrika na kucheza mechi ya mtoano Ili kuwania tiketi ya kuingia makundi ya kombe hilo

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!