Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Michezo Simba ruksa mashabiki Klabu bigwa
Michezo

Simba ruksa mashabiki Klabu bigwa

Spread the love

 

SHIRIKISHO la mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), limeruhusu klabu ya Simba kuingiaza mashabiki, kwenye mchezo wa klabu Bingwa Barani Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy kutoka nchini Botswana kwenye mchezo wa marudiano. Anaripoti Damas Ndelema Tudarco… (endelea)

Mchezo huo wa marudiano, utapigwa tarehe 24 Oktoba 2021, kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, huku idadi kamili ya mashabiki iliyoruhisiwa ikiwa ni 15000.

Simba itaondoka nchini hii leo tarehe 15 Oktoba 2021, kuelekea nchini Botswana kwa ajili ya mchezo wa duru la kwanza dhidi ya Jwaneng Galaxy, utakaopigwa Jumapili tarehe 17 Oktoba 2021.

Aidha taarifa hiyo ya Caf kuruhusu mashabiki imezigusa mpaka klabu za Azam Fc na Biashara United, zinazoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho.

Klabu hizo mbili zitashuka Uwanjani leo na kesho kutupa karata zao kwenye michezo ya mzunguko wa pili wa michuano hiyo.

Kwa upande wa Biashara United, wao hii leo watashuka Dimbani kuwakabili Al Ahly Tripoli kutoka nchini Libya, majira ya saa 9 jioni, kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Jijini Dar es Salaam.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Anza Jumamosi yako na mkwanja wa Meridianbet

Spread the loveJumamosi ya leo ODDS zimekaa kijanja sana ndani ya Meridianbet...

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

error: Content is protected !!