RAIS Samia Suluhu Hassan, ameipa maagizo Wizara ya Katiba na Sheria, ikafanyie kazi madai ya upatikanaji katiba mpya. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).
Agizo hilo la Rais Samia limetolewa leo tarehe 4 Aprili 2024, Ikulu jijini Dar es Salaam, akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, akiwemo Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Jumanne Sagini.
Rais Samia amemtaka Sagini kushirikiana na waziri wake, Dk. Pindi Chana, kufanyia kazi suala hilo.
“Wewe (Sagini) ni mzoefu sana serikalini, utamsaidia mwenzio mambo unayoyafahamu lakini pia sasa nenda kasaidie kwenye katiba na sheria, kipindi hiki tulicho nacho watu wanadai katiba yao nenda kasaidianeni na waziri na imani yangu utaenda kufanya vizuri,” amesema Rais Samia.
Agizo hilo la Rais Samia linajiri baada ya kiongozi huyo kuwaahidi watanzania kwamba mchakato wa upatikanaji katiba mpya utatanguliwa na zoezi la utoaji elimu ya katiba kwa wananchi katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Wadau wengi hususan wa vyama vya siasa na asasi za kiraia, walipinga pendekezo hilo kwa madai kuwa linalenga kupoteza muda na kushauri mchakato huo ufufuliwe mara moja kwa kuwa kazi kubwa ilikwisha fanyika ikiwemo maandalizi ya rasimu za katiba zilizokusanya maoni kutoka kwa wananchi.
Ningekuwa na uwezo ningewaomba wale wachache wenye chama wangekubali Katiba mpya nzuri njema inayojulikana kisomi. Ee Mungu