Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia apangua baraza la mawaziri, Biteko awa Naibu Waziri Mkuu, Silaa aula
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia apangua baraza la mawaziri, Biteko awa Naibu Waziri Mkuu, Silaa aula

Spread the love

 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, kwa kuanzisha nafasi mpya ya Naibu Waziri Mkuu, kuunda wizara mbili na kuhamisha baadhi ya mawaziri. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mabadiliko hayo yametangazwa leo tarehe 30 Agosti 2023 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka.

“Rais ameanzisha nafasi ya Naibu Waziri Mkuu na kuifuta Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na badala yake kuunda wizara mpya mbili ambazo ni Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Uchukuzi.

Aidha, ameimarisha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuongeza nafasi ya Naibu Waziri na Katibu Mkuu watakaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki,” amesema Balozi Kusiluka.

Katika mabadiliko hayo, Rais Samia amemteua aliyekuwa Waziri wa Madini, Dotto Biteko, kuwa Naibu Waziri Mkuu atakayeshughulikia uratibu wa shughuli za Serikali na Waziri wa Nishati.

Katika mabadiliko hayo, Rais Samia ameteua mawaziri wanne, naibu mawaziri watano, makatibu wakuu watatu na naibu makatibu wakuu watatu.

“Vilevile, amewabadilisha wizara baadhi ya mawaziri na makatibu wakuu,” amesema Balozi Kusiluka.

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, sura mpya zilizoingia katika Baraza la Mawaziri ni ya Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa, aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Mbunge wa Misungwi, Alexander Mnyeti, ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Mufindi Kusini, David Kihenzile, akiteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi.

Wengine wapya walioteuliwa ndani ya baraza hilo ni Mbunge wa Viti Maalum mkoani Ruvuma, Judith Kapinga, aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Mbunge wa Mkinga, Dustan Kitandula, aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!