Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali kuwashtaki wanaosambaza picha za wahanga wa ukatili mitandaoni
Habari za Siasa

Serikali kuwashtaki wanaosambaza picha za wahanga wa ukatili mitandaoni

Spread the love

SERIKALI imewaonya watu wanaosambaza mitandaoni picha na video za wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia, ikisema itawashtaki kama hawataacha mara moja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Onyo hilo limetolewa leo tarehe 30 Agosti 2023, bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima, akimjibu swali la Mbunge Viti Maalum CCM, Fatma Taufiq, aliyehoji kauli ya serikali dhidi ya watu wanaosambaza matukio hayo mitandaoni.

“Kuhusu wanaopiga picha mitandaoni kweli inasikitisha sana, Serikali imekuwa ikitoa maelekezo na maagizo kwamba waache kufanya hivyo na wamekuwa wakiendelea. Sasa kauli ya Serikali ni kwamba vitendo hivyo ni vibaya katika malezi na maadili ya taifa, vinaharibu watoto wetu ambao ni taifa la kesho,” amesema Dk. Gwajima.

Dk. Gwajima amesema “Hili ni onyo la mwisho vinginevyo ninakwenda kuita kikao kwa wadau wote na waliopiga picha za namna hiyo nitawaongoza kwenda kuwashtaki kwa mujibu wa sheria kwenye Jeshi la Polisi, ili sheria zetu tulizotunga wenyewe zifanye kazi.”

Swali la Taufiq lilitokana na swali la msingi lililoulizwa na  Mbunge wa Viti Maalum CCM, Martha Gwau, aliyehoji Serikali ina mpango gani kuhusu ujenzi wa nyumba za kuwahifadhi waliofanyiwa vitendo vya ukatili, akidai vimeongezeka kwa kasi.

Dk. Gwajima alijibu swali hilo akisema Serikali imeandaa muongozo wa uanzishaji na uendeshaji wa nyumba salama wa 2019, kwa ajili ya manusura wa vitendo hivyo, pamoja na wahanga wa biashara haramu ya usafirishaji binadamu. Ambapo hadi sasa nyumba 12 zimejengwa na kusajiliwa kwenye mikoa ya Mwanza, Kigoma, Kilimanjaro na Dar es Salaam.

Aidha, Dk. Gwajima amesema Serikali itaendelea kutenga fedha katika bajeti zake, kwa ajili ya kujenga nyumba hizo, huku akitoa wito kwa mamlaka za serikali za mitaa na wadau mbalimbali, kuiunga mkono.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!