Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia amteua Zuhura Yunus kuwa mkurugenzi wake wa Mawasiliano
Habari za Siasa

Rais Samia amteua Zuhura Yunus kuwa mkurugenzi wake wa Mawasiliano

Zuhura Yunus
Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa mwandishi na mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Zunura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Zuhura ambaye ni Mtanzania anachukua nafasi ya Jaffar Haniu ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Zuhura ambaye ameitumikia BBC kwa miaka 14, hivi karibuni alitangaza kuachia ngazi ndani ya shirika hilo kubwa duniani.

Taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu aliyoitoa leo Jumanne, tarehe 1 Februari 2022 imeeleza uteuzi huo umeanza 30 Januari 2022.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!