RAIS Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kutokana na kifo cha aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Jecha ambaye aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuanzia tarehe 30 Aprili 2013 hadi tarehe 29 Aprili 2018, amefariki dunia leo Jumanne katika Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
Aidha, kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, Rais Samia imesema;
“Rais Samia amepokea taarifa za kifo cha marehemu Jecha kwa majonzi makubwa na masikitiko makubwa,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Mbali na salamu kuhusu msiba wa Jecha, Rais Samia pia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Rais wa awamu ya tatu, Hayati Benjamin Mkapa, kutokana na kifo cha Bernard Mkapa (kaka wa Hayati Benjamin Mkapa).
“Rais Samia amewaomba wanafamilia wote wawe na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na anawaombea marehemu wote wapumzike mahali pema peponi, Amina,” imeeleza taarifa hiyo.
Leave a comment