Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Kikwete afunguka misukosuko anayokumbana nayo Rais Samia
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Kikwete afunguka misukosuko anayokumbana nayo Rais Samia

Spread the love

RAIS Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete, amesema anaridhika na uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, hususan utulivu wake anaouonesha katika kipindi ambacho Serikali yake na changamoto nyingi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari, leo Jumanne, jijini Arusha, Kikwete amesema “nafasi ile (urais) ngumu, sio rahisi. Ina changamoto nyingi unaweza ukaamua hili likaleta kelele nyingi, lakini inategemea na uongozi wako unavyoliongoza taifa.”

“Mimi kwa kweli naridhika, anaongoza nchi vizuri, mtulivu, hana hamaki, hana hasira na unajua kitu kikubwa kwenye uongozi ni utulivu. Nafurahi amekuwa mtulivu, nchi haiwezi kupoa kama ugali kwa hiyo nadhani naridhika nalo,” amesema Dk. Kikwete.

Kiongozi huyo mstaafu wa Tanzania ametoa kauli hiyo alipoulizwa kama ana imani na utendaji wa Rais Samia, aliyeingia madarakani Machi 2021, kufiatia kifo cha mtangulizi wake, Hayati John Magufuli, ambapo alijibu kuwa ana imani naye huku akisema misukosuko anayokutana nayo,  hata yeye iliwahi kumkuta alivyokuwa rais.

“Mi nimepitia misukosuko mingi tu, nimeingia tu kuna msukosuko wa EPA, nilivyokwenda tukaja Richmond, mara Dowansi ndiyo uongozi wa nchi unavyokuwa. Tukaja Escrow, changamoto hizo ni za kawaida lakini ni jinsi gani katika kipindi hicho kiongozi anaongoza taifa katika mazingira yenye changamoto nyingi,” amesema Dk. Kikwete.

Akielezea namna alivyomfahamu Rais Samia, Dk. Kikwete amesema alianza kujua uwezo wake alipokuwa naye katika timu iliyoundwa 2001 kwenda katika mataifa ya nje kuelezea hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania, kutuliza machafuko yaliyotokana na uchaguzi mkuu wa 2020.

Amesema wakati timu hiyo inatekeleza majukumu yake, alifanikiwa kuuona uwezo mkubwa wa kiuongozi wa Rais Samia, kitendo kilichomshawishi amteuae kuwa waziri alipoingia madarakani.

Pia, alimshawishi Hayati Magufuli, akubali awe mgombea mwenza katika uchaguzi wa kiti cha urais wa 2015, ambapo alishinda kisha mwanamama huyo kufanikiwa kuwa makamu wa rais.

Licha ya kutoweka bayana misukosuko anayokumbana nayo Rais Samia, lakini kwa sasa serikali yake inakabiliana na upinzani mkali kuhusu uamuzi wake wa kushirikiana na Serikali ya Dubai katika uendeshaji bandari nchini.

Tangu mkataba wa ushirikiano huo uridhiwe na Bunge kwa ajili ya utekelezaji, makundi mbalimbali hususan ya kisiasa, yaliibuka kupinga uwekeza huo kwa madai kuwa unakiuka katiba ya nchi na haulindi maslahi ya taifa.

Hata hivyo, Serikali ya Rais Samia mara kadhaa imetoka hadharani na kutoa ufafanuzi ikisema mkataba huo una tija kwa Taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari za Siasa

Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25

Spread the loveWIZARA ya Kilimo, imepanga kutumia bajeti ya Sh. 1.2 trilioni...

error: Content is protected !!