Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mahakama: Afande Rama hana hatia
Habari MchanganyikoTangulizi

Mahakama: Afande Rama hana hatia

Spread the love

Mahakama ya Mkoa wa Vuga mjini Unguja imemwachia huru mshtakiwa Ramadhan Ali maarufu kama Afande Rama aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka ya kuingiliwa kinyume na maumbile. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Afande Rama ameachiwa huru leo Jumanne  baada ya hakimu wa mahakama hiyo, Khamis Simai kudai kuwa mshtakiwa hana hatia chini ya kifungu cha 220 ya sheria namba 7 ya mwaka 2018.

Kesi hiyo namba 59 ya mwaka 2023 ilianza kusikilizwa mahakamani hapo ambapo jumla ya mashahidi tisa kutoka upande wa mwendesha mashtaka waliwasilisha ushahidi wao ambao hawakuweza kumtia hatiani mtuhumiwa.

Ramadhani alishtakiwa baada ya kusambaa kwa video katika mitandao ya kijamii zilizodhaniwa kuwa ni yeye ambaye alionekana akishiriki tendo la kuingiliwa kinyume na maumbile.

Upande wa mashtaka ulikuwa unawakilishwa na muendesha mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Mohd Saleh.

Afande Rama ambaye alikuwa Askari wa kikosi cha kutuliza gasia, kabla ya kushtakiwa, alivuliwa cheo cha uaskari na kubaki raia wa kawaida.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

error: Content is protected !!