May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia akemea kutumia nguvu kukusanya kodi, kuzifungia akaunti

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amekerwa na kitendo cha matumizi ya nguvu katika kukusanya kodi ikiwemo kuzifungia akaunti za wafanyabiashara na kuchukua fedha zao. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Amemtaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba kwenda kuongoza vyema wizara hiyo ikiwa ni pamoja na kutanua wigo wa ukusanyaji kodi kwa kuanzisha vyanzo vipya.

Rais Samia, ametoa kauli hiyo leo Alhamisi tarehe 1 Aprili 2021, mara baada ya kumaliza kuwaapisha mawaziri, naibu mawaziri na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga, Ikulu ya Chamwino, Dodoma ambao aliwateua jana Jumatano.

Dk Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kauli hiyo ameitoa, baada ya Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Philip Mpango, kumtaka Dk. Nchemba kuweka mikakati ya kuhakikisha hadi kufikia mwisho wa mwaka 2021, makusanyo kwa mwezi yafikie Sh.2 trilioni kutoka Sh.1 trilioni.

“Nendeni mkatanue wigo wa kodi na mtengeneze walipa kodi wengi zaidi, trend mnayoenda nayo ni kuua walipa kodi na mnaua wafanyabiashara kwa kutumia nguvu zaidi kuliko akili na maarifa kupata kodi.”

“Sasa wale mnaowakamua, mkienda mkachukua vifaa vyao vya kazi, mkafungia akaunti zao, mkachukua fedha zao kwa nguvu kwenye akaunti, kisa sheria inakuruhusu kufanya hivyo, akitoka hapo anahamia nchi nyingine, mnapunguza walipa kodi. Nendeni mkatanue walipa kodi,” amesema Rais Samia

error: Content is protected !!