JUMLA ya watu watano wanaidaiwa kufariki dunia katika vijiji vya Bulinda na Butayaibega vilivyopo kata ya Maruku na Kanyangereko wilaya ya Bukoba vijijini mkoani Kagera kutokana na ugonjwa ambao haujafahamika huku dalili zake zikiwa ni kutokwa na damu maeneo mbalimbali ya mwili. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 16 Machi na Mganga Mkuu wizara ya Afya, Prof. Tumaini Nagu, jumla ya watu saba wanasadikika walipata dalili za homa ya ugonjwa huo. Mbali na homa dalili nyingine zinatajwa kuwa ni kutapika, kutokwa damu maeneo mbalimbali ya mwili na figo kushindwa kufanya kazi.

Taarifa hiyo imesema watu watano kati yao wamefariki na wengine wawili wako hospitali wanaendelea na matibabu.
Amesema mwenendo wa ugonjwa huu unaashiria uwezekano kuwa ni ugonjwa wa kuambukiza.
Amesema Serikali inaendelca kufuatilia kwo karibu kuhusu mwenendo wa ugonjwa huo na kuchukua hatua za kudhibiti ili usisambae.
Ametaja hatua hizo kuwa ni pamoja na; sampuli kutoka kwa wagonjwa na waliofariki zimechukuliwo ili kubaini chanzo na kuthibitisha aina ya ugonjwa huo.
“Ufuatiliaji wa watu wenye viashiria vya ugonjwa kwenye jamii na vituo vya kutoa huduma za afya pamoja na waliotangamana na wagonjwa hao ili kuwapa huduma stahiki za kimatibabu.
“Timu za kitaalamu za kukabiliana na mlipuko ngazi ya mkoa na halmashauri zimetumwa katika maeneo yaliyoathirika na zinaendelea na uchunguzi na hatua za udhibiti.
“Dawa, vifaa na vifaa tiba muhimu vipo katika vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Kagera na wagonjwa wanaendelea na matibabu.
“Elimu ya afya inaendelca kutolewa kwa jamii katika mkoa wa Kagera ili kuchukua tahadhari,” amesema Prof. Nagu.
Aidha, amesema wakati Serikali inafuatilia mienendo wa ugonjwa na kuchukua hatua za udhibiti, amewataka wananchi muendelea kuwa watulivu na kuchukua hatua mbalimbali.
Ametaja hatua hizo kuwa mtu yeyote mwenye dalili za homa, kutapika, kuharisha, kutoka damu na mwili kuishiwa nguvu anashauriwa kuwahi kituo cha kutolea huduma za afya mapema kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.
“Kutoa taarifa mapema kwenye kituo cha kutolea huduma kilicho karibu au kupiga simu namba 199 bila malipo endapo utamuona au kukutana na mtu msvenge dalili kamahizo.
“Kuepuka kumgusa mgonjwa au majimaji ya mwili, mate, machozi, damu, mkojo na kinyesi yatokayo kwa mgonjwa au mtu yeyote mwenye dalili hizo,” amesema.
Ameongeza kuwa iwapo itakulazimu kumhudumia mgonjwa kwa dharura, inabidi kuchukua tahadhari ya kujikinga na majimaji yoyote kabla ya kumhudumia.
Inabidi pia kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono ili kujikinga na magonjwa yote ya kuambukiza.
Pia kepuuka kusalimiana kwa kushikana mikono pamoja na kushirikisha wataalam wa afya katika shughuli za misiba na mazishi katika kipindi hiki.
Aidha, Prof Nagu amewakumbusha watumishi wa afya kuzingatia kanuni za kujikinga na magoniwa ya kuambukiza (IPC) wakati wa kutoa huduma.
Pamoja na mambo mengine amesema Serikali inatoa pole kwa familia zilizoondokewa na wapendwa wao.
“Aidha, nihitimishe kwa kuwaondoa hofu watu wote na kuwaomba kuwa watulivu wakati Wizara inaendelca kufuatilia kwa karibu na kuchukua hatua za udhibiti. Tutaendelea kuwapa taarifa za mwenendo wa ugonjwa huu,” amesema.
Leave a comment