Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Shule ya Hazina yaanza kutoa elimu bure
ElimuHabari

Shule ya Hazina yaanza kutoa elimu bure

Shule ya Hazina ya Magomeni jijni Dar es Salaam imeanza kutoa elimu ya awali bure kuanzia Baby class, middle class na Pre Unit kwa miezi mitatu. Picha hii inamwonyesha Mkuu wa shule hiyo Omar Juma, akimpa zawadi mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo Iptusm Ramadhani aliyekuwa wa kwanza kwenye mtihani wa utamilifu shuleni hapo katika mtihani uliofanyika katikati ya na shule hiyo kufanikiwa kuwa ya kwanza Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Spread the love

KATIKA jitihada za kuunga mkono serikali ya awamu ya sita katika utoaji wa elimu, Shule Kimataifa ya Hazina ya Magomeni jijini Dar es Salaam imeanza kutoa elimu ya awali bure. Anaripoti Mwandishi Wetu….(endelea)

Elimu hiyo ya bure inatolewa kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Oktoba, Nobemba hadi Desemba kwa wanafunzi wa shule ya awali kuanzia chekechea yaani baby class, Middle Class na Pre Unit.

Mkuu wa shule hiyo, Juma Omar alisema watakachochangia wazazi wa wanafunzi hao ni chakula na sare za shule pekee ila hawatatozwa ada.

Akizungumza kwa nini shule hiyo imeamua kutoa elimu hiyo bure, mwalimu Omar alisema wameamua kurejesha sehemu ya faida kwa jamii kwa kuwaamini kwa miaka mingi.

Alisema wazazi wameiamini shule hiyo kwa muda mrefu na kuwapa wanafunzi kila mwaka hivyo wameaona watoe zawadi ya elimu hiyo bure kama motisha kwao.

Shule ya Hazina imeanza kutoa elimu bure awali kuanzia baby class, Middle na Pre Unit. Picha iliyopigwa Septemba 29 inaonyesha Mkuu wa taaluma wa shule ya msingi Hazina ya Magomeni jijini Dar es Salaam, Wilson Otieno akimpa tuzo mwanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo, Blessing Mayongo kwa aliyefanikiwa kuongoza kwenye matokeo ya shule hiyo ya mtihani wa utahimilifu (moko) kwa kupata alama 293 kati ya 300 zinazotakiwa mwezi uliopita .

“Tungependa wazazi waje waone tunafanya nini hadi tunaongoza wilaya ya Ilala na wakati mwingine Mkoa wa Dar es Salaam kwenye mitihani ya kitaifa,” alisema

Aidha, alisema baadhi ya wazazi wameanza kuitikia wito huo na kuanza kupeleka watoto wao na kwamba shule hiyo itaakauwa na uwezo hata wakupokea wanafunzi zaidi ya 100 kama watajitokeza.

“Hazina inawashukuru wazazi ambao wametuamini kwa muda mrefu na tunawaomba waendelee kutuamini kwa kutuletea watoto wao na wachangamkie fursa hii ya masomo bure hadi Desemba,” alisema

Aliahidi kuwa shule hiyo itaendelea kufanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa kutokana na mazingira mazuri ya kusomea na ari ya ufundishaji ya walimu wa shule hiyo.

Mmoja wa wazazi, Halima Hussein, alisema yeye kama mzazi amefurahishwa na hatua hiyo ya Hazina kwani inawapa moyo wazazi na itawasaidia wale wasio na uwezo kupeleka watoto wao.

Shule ya Kimataifa Hazina ya Magomeni jijini Dar es Salaam imeanza kutoa elimu bure katika kuunga mkono juhudi za seriali ya awamu ya sita. Picha hii ya Septemba 29 mwaka huu inawaonyesha waliokuwa wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Hazina ya Magomeni Dar es Salaam walipokuwa kishangilia baada ya wote kupata alama A kwenye mtihani wa utahimilifu (moko) matokeo yaliyotoka mwezi wa tisa.

“Hii ni mara ya kwanza kusikia shule ya kimataifa na bora kama Hazina inatoa ofa ya aina hii kwa hiyo nawashauri wenzangu wachangamkie fursa hii kwa kuwaandikisha watoto wao wanufaike na elimu bure,” alisema Halima

Minza Mulele kwa upande wake alisema kwa shule hiyo kuamua kutoa elimu bure kwa miezi mitatu ni jambo la kupongezwa na linalopaswa kuigwa na shule zingine.

“Shule zisiangalie faida tu kila wakati zinapaswa kutoa huduma wakati mwingine ndiyo maana nawapongeza sana Hazina kwa uamuzi huu wa kutoa elimu bure kwa miezi mitatu,” alisema Mulele.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

ElimuMakala & Uchambuzi

Waraka maalumu kwa NECTA, “hawapaswi kuungwa mkono”

Spread the loveHATUA iliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), ya...

Elimu

NACTVET yafungua dirisha la udahili

Spread the love  BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo...

Elimu

Prof. Mwakalila awafunda wanafunzi Chuo Mwalimu Nyerere, “ulipaji ada ni muhimu”

Spread the love  MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere (MNMA),...

error: Content is protected !!