Tuesday , 26 September 2023
Home Kitengo Habari Benki ya NBC yazindua kombe jipya la Ligi Kuu Tanzania Bara
HabariMichezo

Benki ya NBC yazindua kombe jipya la Ligi Kuu Tanzania Bara

Spread the love

MDHAMINI Mkuu wa Ligi ya NBC , Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) leo Jumatano imezindua kombe jipya la ligi kuu ya soka ya Tanzania bara lililoboreshwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mkurugenzi wa fedha wa Bodi ya Ligi, Ibrahim Mwayela (wa pili kushoto) akilifurahia kombe jipya la ligi kuu ya soka Tanzania bara lililoboreshwa baada ya kuzinduliwa rasmi na mdhamini mkuu benki ya NBC. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa NBC benki.

Kombe hilo ambalo limezinduliwa mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam litakabidhiwa kwa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania mara kwa msimu huu na misimu ijayo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa benki hiy,o Godwin Semunyu alisema  benki ya NBC ikiwa kama mdhamini mkuu wa ligi imeboresha kombe kutokana na maoni ya wadau mbalimbali mbali wa soka.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa Umma wa benki ya NBC, Godwin Semunyu (kulia) akilifurahia kombe jipya la ligi kuu Tanzania bara na mkurugenzi wa fedha wa bodi ya ligi Ibrahim Mwayela (kushoto) wakati wa uzinduzi rasmi wa kombe hilo lililoboreshwa jijini Dar es Salaam

“NBC ikiwa mdhamini mkuu wa ligi ya Tanzania bara inajivunia mafanikio makubwa ya ligi yetu. Kwa sasa ligi yetu ni ya tano kwa ubora Afrika nah ii ni hatua kubwa na nzuri kwa soka letu. Leo tumezindua kombe lililoboreshwa ikiwa pia ni sehemu ya kuongeza thamani kwa ligi yetu,” alisema.

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC wakiwa katika picha ya pamoja na wageni wengine waalikwa wakati wa uzinduzi wa kombe jipya lililoboreshwa la ligi kuu ya NBC Tanzania bara.

Godwin aliongeza kuwa, ikiwa ni sehemu ya maboresho ya ligi, benki ya NBC inatoa bima kwa wachezaji wote wa ligi kuu pamoja na familia zao na pia mikopo ya mabasi kwa timu zinazoshiriki ligi.

Baadhi ya wafanyakazi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiwa katika picha ya pamoja na wageni wengine waalikwa wakati wa uzinduzi wa kombe jipya lililoboreshwa la ligi kuu ya NBC lililozinduliwa jijini Dar es Salaam.


“Ili kuongeza hamasa kwa wachezaji na makocha, tunatoa tuzo mbali mbali kwa makundi haya kila mwezi. Benki ya NBC itaendelea kutoa mchango wake katika kusaidia maendeleo ya michezo hapa nchni kwa kuwa inatambua umuhimu na mchango wa michezo kwa maendeleo,” aliongezea

Kwa upande wake Mkurugenzi wa fedha wa Bodi ya ligi, Ibrahim Mwayela alisema  udhamini wa NBC umekuwa wenye tija kubwa kwa ligi na kuongeza kuwa NBC ni mdau mkubwa katika maendeleo ya soka hapa nchini.

‘Leo Tanzania tunajivunia ligi yetu kuwa moja katika ligi bora barani Afrika tukishikilia nafasi ya tano. Tunaishukuru sana benki yaNBC kwa udhamini wake ambao umesaidia kufika hapa tulipo huku tukisonga mbele kwa  kujiamini,” alieleza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMichezo

Piga pesa kupitia Derby ya London Kaskazini kwa kubadhiri na Meridianbet

Spread the love NAJUA umesikia na unazijua Derby nyingi kutoka jiji la London,...

BiasharaMichezo

Wikiendi hii ushindi upo Meridianbet na si kwingine

Spread the love USHINDI huu ni wako mteja wa Meridianbet kama mechi...

BiasharaMichezo

Safari ya Gavi kutoka Academy ya Real Betis mpaka Barca

Spread the love  ANITWA Pablo Martín Páez Gavira ‘Gavi’, sasa ni mchezaji...

BiasharaMichezo

SBL yazindua Serengeti Oktoba Festival

Spread the love  KAMPUNI ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) kupitia...

error: Content is protected !!