Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia afanya uteuzi akiwa Scotland
Habari Mchanganyiko

Rais Samia afanya uteuzi akiwa Scotland

Spread the love

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Dk. Nicolaus Shombe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kabla ya uteuzi huo, Dk. Shombe alikuwa Kamishna wa Mipango- Wizara ya Fedha na Mipango.

Dk. Shombe, anachukua nafasi ya Profesa Damian Gambagambi ambaye alifariki dunia Jumanne ya tarehe 20 Oktoba 2020, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam

Uteuzi huo, umeanza tarehe 29 Oktoba 2021.

Taarifa ya uteuzi wake, imetolewa jana Jumatatu, tarehe 1 Novemba 2021 na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Rais Samia amefanya uteuzi huo akiwa Glasgow nchini Scotland anakohudhulia mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi (CPO26).

Mkutano huo, umeanza jana Jumatatu na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa nchi na leo Jumanne, Rais Samia anatarajia kuhutubia mkutano huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

error: Content is protected !!