MKUTANO wa Tano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, unatarajiwa kuanza kesho tarehe 2 Novemba, mwaka 2021 huku matumizi ya fedha za mkopo nafuu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwa ajili ya kukabiliana na athari za UVIKO-19 yakitarajiwa kujadiliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi Bunge leo tarehe 1 Novemba, 2021 imebainisha kuwa shughuli kubwa kesho itakayofanyika katika Ukumbi wa Msekwa ni Bunge kupokea maelezo kuhusu maeneo ya vipaumbele ya matumizi kuhusu fedha hizo.
Aidha, kwa mujibu wa ratiba hiyo, siku ya Jumatano tarehe 3 Novemba, 2021 Kamati ya Mipango itawasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023.
Mapendekezo ya mpango huo yatajadiliwa kwa muda wa siku tano kabla ya Bunge kupokea maelezo kuhusu miradi ya nishati ya umeme ya kimkakati na hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wake.
Bunge hilo litaahirishwa tarehe 12 Novemba mwaka huu.
Leave a comment