May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Mwinyi: Nileteeni anayefanana na Maalim Seif

Spread the love

 

SIKU chache baada ya Maalim Seif Shariff Hamad (71), aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais visiwani humo kufariki dunia, Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, alizuru kwenye msikiti wa maalim na kueleza sifa za mrithi amtakaye serikalini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

“Rais Mwinyi alikwenda kwenye msikiti aliojenga Maalim Seif, alikutana na wazee wa pale na katika kuogea, alituma ujumbwe kwa ACT-Wazalendo, kwamba anaomba achaguliwe mtu kama Maalim Seif,” ameeleza Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo.

Zitto ametoa kauli hiyo leo Jumatatu tarehe 1 Machi 2021, akizungumza na Kituo cha Televisheni cha Clouds cha 360.

Amesema, tayari chama hicho kimekutana kujadili na kupendekeza jina la Makamu wa Kwanza wa Rais visiwani huo.

“Nafasi hii sio ya kugombewa, ni ya kuteuliwa na tumekaa kikao Ijumaa tumemaliza siku hiyo na kuwasilisha jina mara moja. Uamuzi wa uteuzi ni ya rais,” amesema.

 

Hata Zitto alipotakiwa kueleza jina la mteule wa Maalim Seif, amesema mamlaka ya uteuzi ni ya rais na kwamba, kazi kwao ilikuwa ni kuwasisha jina tu.

Akizungumzia sifa za mteule huyo, Zitto amesema aliyeteuliwe anazo sifa ambazo Maalim Seif, aliyekuwa mwenyekiti wa ACT-Wazalendo alizipendekeza kwa mrithi wake.

Amesema, sifa hizo ni pamoja na kuwa na dhamira ya maridhiano na jasiri kama ambavyo, Maalim Seif alivyopendekeza.

Kiongozi huyo amesema, Maalim Seif aliandaa vijana wengi wa kumrithi, na kazi hiyo aliianza muda mrefu. Na kwamba, wengine walitaka haraka kufikia malengo na hawakuwa na subra hivyo wakaondoka.

“Katika uteuzi huu, tulizingatia wosia wake, ingawa mwalimu (Maalim Seif) alitupa ishara lakini tulimwangalia kama anatimiza vigezo,” amesema Zitto.

Maalim Seif Sharrif Hamad, aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo

Amesema, Maalim Seif alikuwa akiona anaelekea mwishoni mwa hekaheka za siasa, na hata kwenye uchagazi mkuu 2020, alipendekeza majina ya watu aliotaka wagombee urais tofauti na yeye (Maalim Seif).

Zitto amesema, hata wale waliopendekezwa kuwa nauwezo wa kushika nafasi hiyo baada ya kuwaandaa kwa muda mrefu, nao walitaka Maalim Seif kusimama katika uchaguzi huo kama mgombea urais.

“Maalim alikuwa na vijana wengi amewaandaa, inagwa wanazidiana lakini wameandaliwa. Hata kwenye uchaguzi uliopita alitaka mmoja agombee, lakini walimtaka mwenyewe (Maalim Seif) agombee,” amesema Zitto.

Akizungumzia maisha ya ACT-Wazalendo baada ya Maalim Seif, Zitto amesema mpaka sasa chama hicho bado kina mshikamano na hakuna viashiria vyovyote.

error: Content is protected !!