May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bumbuli huru, ashinda rufaa yake

Hassan Bumbuli, Afisa Habari na Mawasiliano wa Yanga

Spread the love

 

AFISA habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli ameshinda rufaa yake mara baada ya kufungiwa miaka mitatu kujihusisha na masuala ya mpira wa miguu mara baada ya kushindwa kulipa kiasi cha Sh. 5,000,000. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Bumbuli alifungiwa na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tarehe 27 Januari 2021, kujihusisha na masuala ya mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka mitatu kwa kushindwa kulipa kiasi cha shilingi milioni tano kama sehemu ya adhabu mara baada ya kukutwa na hatia.

Jana Kamati ya Rufaa ya TFF ilitengua adhabu hiyo baada ya Bumbuli kukataa rufaa siku chache toka alipofungiwa na kutoa vielelezo vya kwamba ameshalipa kiasi hiko cha pesa.

Kwa sasa Bumbuli anarejea kwenye majukumu yake kama Afisa habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga.

Afisa habari huyo alitiwa hatiani kwa kutoa maneno yasiofaa kwa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuhusu sakata la mchezaji Bernard Morrison kwenye kesi yake ya kimkataba dhidi ya klabu yake ya zamani ya Yanga.

error: Content is protected !!