Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Mwinyi aipongeza NMB kuchangia maendeleo Zanzibar
Habari za Siasa

Rais Mwinyi aipongeza NMB kuchangia maendeleo Zanzibar

Spread the love

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Benki ya NMB kwa kuendelea kuunga mkono ajenda ya maendeleo endelevu Visiwani Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akizungumza mara baada ya kushiriki katika matembezi ya sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar yaliyofanyika Zanzibar Mjini, Dk. Mwinyi aliipongeza benki hiyo huku akibainisha kuwa msaada wa Benki ya NMB umekuwa chachu katika kukuza uchumi, na kuleta maendeleo endelevu Visiwani humo.

“Benki ya NMB imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Serikali yetu katika kuchochea maendeleo ya sekta mbalimbali za Zanzibar. Natumia fursa hii kuipongeza benki ya NMB kwa kuendelea kutuunga mkono na ningependa kuchukua fursa hii kuyaomba mashirika mengine yanayofanya kazi Visiwani hapa kuunga mkono ajenda yetu ya maendeleo,” amesisitiza Rais Mwinyi.

Awali, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Tabia Maulid Mwita naye aliimwagia sifa benki hiyo na kuongeza kuwa benki hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika kukukuza maendeleo ya sekta ya michezo Visiwani Zanzibar.

Mwita alishukuru benki hiyo kwa kushiriki kikamilifu katika matembezi ya sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar baada ya benki hiyo kutoa udhamini wa shilingi milioni 200 wa vifaa vya michezo hivi karibuni.

Alisisitiza dhamira ya Wizara ya kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa Zanzibar ili kuimarisha maendeleo ya michezo.

Naye Meneja wa Bashara ya Zanzibar wa Benki ya NMB, Naima Said Shaame wakati wa hafla hiyo alisisitiza dhamira ya benki hiyo ya kuendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Sulaiman Abdulla (kushoto) akisalimiana na Meneja wa Biashara ya Zanzibar wa Benki ya NMB, Naima Said Shaame (kulia) muda mfupi kabla ya kuanza kwa matembezi ya hisani katika tamasha la Mazoezi ya viungo kitaifa. Katikati ni waziri wa Nchi ofisi ya Rais, Kazi uchumi na uwekezaji wa Serikali ya Zanzibar, Mudrik Soraga

Pia aliongeza kuwa benki hiyo mbali na kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo imekuwa na mchango mkubwa katika kuwekeza katika uwekezaji wa kijamii wa kijamii (CSIs) ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kukuza thamani ya wadau wake wote ikiwa ni pamoja na jamii ambako benki inafanyia kazi.

“Sisi kama benki, tutaendelea kuunga mkono kikamilifu utekelezaji wa Ajenda ya Uchumi wa Bluu ya Serikali ya Zanzibar kupitia utoaji wa huduma bora za kibenki ninazokidhi matakwa ya wateja wetu,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!