June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Afghanistan: Narudi nyumbani, sikuiba pesa

Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani

Spread the love

RAIS wa Afghanistan, Ashraf Ghani ambaye alikuwa akiongoza nchi ya hiyo kabla ya kundi la Taliban kuiteka mapema wiki hii, amehutubia taifa hilo na kusema anatarajia kurejea nyumbani.

Rais Ghani ambaye alitoroka nchi yake na kuelekea katika nchi za falme za kiarabu – UAE amesema hana mpango wa kuishi huko kwa sababu Kabul ndio nyumbani kwake.

Pia amekanusha madai ya kutoroka na fedha dola za Marekani milioni 169.

Ghani ametoa kauli hiyo jana Agosti 18, wakati akihutubia wananchi wa Afghanistan kufuatia madai mbalimbali yaliyoibuka dhidi yake.

Amesema wakati anatoroka, hakuweza kuvaa hata viatu bali alivaa sendoz pekee na hakubeba fedha zozote wala hata za kujikimu.

error: Content is protected !!