May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zitto: Hatujitoi Serikali ya Umoja wa Kitaifa, tunarudi Konde

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo

Spread the love

KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema chama hicho hakina mpango wa kujitoa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK). Anaripoti Gabriel Mushi, Dar es Salaam … (endelea).

Pia amesema chama hicho kinatarajia kurejea kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Konde Visiwani Zanzibar.

Uchaguzi huo unatarajiwa kurudiwa baada ya aliyekuwa mbunge mteule wa jimbo hilo, Sheha Mpemba Faki (CCM) kujiuzulu Agosti 2 mwaka huu.

Zitto ametoa kauli hiyo jana Agosti 18 wakati akizungumza na viongozi wa mikoa 11 kichama katika Kisiwa cha Unguja wa chama hicho kuwaeleza maamuzi na maazimio ya Kamati Kuu ya Dharura iliyokutana hivi karibuni.

“Tumewafafanulia masuala ambayo Maalim Seif na Rais Dk. Hussein Mwinyi walikubaliana kabla ya kuingia kwenye serikali ya umoja wa kitaifa… ambayo ni tume ya maridhiano, uchunguzi wa matukio yaliyotokea kwenye uchaguzi mkuu na mabadiliko kwenye sheria za uchaguzi. Hayo ndio tulikuwa tunawaeleza wananchi wetu,” alisema Zitto.

Kauli hiyo ya Zitto imefuta minong’ono iliyoibuka hivi karibuni kwamba Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Othman Masoud kutoka ACT Wazalendo, anatarajia kujitoa SUK.

error: Content is protected !!