Friday , 9 June 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Raila Odinga: Tutafanya maandamano makubwa mara mbili kwa wiki
Kimataifa

Raila Odinga: Tutafanya maandamano makubwa mara mbili kwa wiki

Spread the love
KIONGOZI wa upinzani nchini Kenya, Raila Amollo Odinga ametangaza kuwa muungano wa Azimio la Umoja (One Kenya), sasa utafanya maandamano makubwa mara mbili kwa kila wiki. Idhaa ya Kiswahili ya BBC, inaripoti kutoka Kenya … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari, muda mfupi uliopita, Raila alieleza kuwa watakuwa wakiingia mitaani kila siku za Jumatatu na Alhamisi, kila wiki hadi matakwa yao yatakaposikilizwa na kushughulikiwa.

Alisema, “katika kukabiliana na matakwa ya umma, kuanzia wiki ijayo, sasa tutafanya maandamano kila Alhamisi na Jumatatu.”

Alikemea nguvu iliyotumiwa na maafisa wa polisi jana Jumatatu, ambapo viongozi kadhaa wakuu wa Azimio na wafuasi wao walikamatwa, na polisi wakazima ndoto yao ya kuandamana hadi Ikulu ya Nairobi.

Mapema jana Jumatatu – 20 Machi 2023 – Raila aliwaambia wananchi, katika kitongoji cha Kamukunji, kwamba “hatua hiyo ya maandamano haitaisha hadi Wakenya wapate kile ambacho ni chao kwa haki.”

Aliongeza, “tumeanza vita. Kila Jumatatu kutakuwa na mgomo. Kutakuwa na maandamano. Vita imeanza na haitaisha mpaka waKenya wapate haki yao.”

Raila Odinga

 

Waziri Mkuu huyo wa zamani  aliwaamuru wafuasi wake kususia bidhaa kadhaa, ikiwa ni pamoja na chombo kimoja cha habari, benki moja ya kitaifa na kampuni moja ya simu.

Raila ndiye mwanasiasa pekeee wa Kenya aliyehai, ambaye amewahi kushikilia cheo cha waziri mkuu nchini humo. Alitanguliwa na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta, ambaye aliyeshika wadhifa huo kati ya mwaka 1963 na 1964 baada ya Kenya kupata uhuru.

Aidha, Raila ndiye mwanasiasa pekee aliyehai ambaye katwikwa shani ya kuitwa baba wa demokrasia ya vyama vingi, sawia na marehemu Keneth Matiba.

Lakini swali la kujiuliza, ni hili: Ni vipi, kwa mara ya tano, Raila ameshindwa kwenye uchaguzi wa Urais? Kwa nini kila ashindwapo, hulalamika kuibiwa kura na kuita wafuasi wake kuandamana kila baada ya uchaguzi wa urais?

Maandamano hayo yamekuwa na faida zozote kwa wafuasi wake, kwa taifa lake; na au hata kwake binafsi? Je, huyu Raila, ameanzia wapi siasa hizo za maandamano?

Endelea kusoma MwanaHALISI Online kwa taarifa zaidi

4 Comments

  • @THINK/Dedication/Remember/DREAMS”@ EMPLOY/US THEM ALL – ALL TANZANIAN HAS JOB TO DO

    In 2021, the unemployment rate in Tanzania remained nearly unchanged at around 32.74 percent. With a decline of 0.04 percentage points, there is no significant change to 2020. Over the observed period, the unemployment rate has been subject to fluctuation.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Kagame afumua tena Jeshi, awafuta kazi maofisa zaidi ya 200 wakiwemo majenerali

Spread the love  RAIS wa Rwanda, Paul Kagame, amewafuta kazi Meja Jenerali...

Kimataifa

Urusi imelipua bwawa kuu la umeme nchini Ukraine

Spread the loveSERIKALI mjini Kyiv nchini, Ukraine imeushutumu utawala wa Rais Vladimir...

Kimataifa

Rais Kagame afanyia mabadiliko makubwa jeshi, usalama wa taifa

Spread the loveRAIS wa Rwanda, Paul Kagame amefanye uteuzi wa wakuu wapya...

Kimataifa

Miili ya waliofariki kwenye ajali ya treni India, kukabidhiwa baada ya vipimo vya DNA

Spread the love  TAKRIBANI watu 260 wamefariki na wengine karibu 650 wamejeruhiwa...

error: Content is protected !!