Wednesday , 1 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Putin apata pigo, Waziri wa ulinzi ajiuzulu
Kimataifa

Putin apata pigo, Waziri wa ulinzi ajiuzulu

Spread the love

NI pigo kwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin baada ya Naibu Waziri wa Ulinzi kutoka nchini Belarusi kujiuzulu wadhifa wake kwa kile alichodai kuwa hawezi kumuunga mkono Putin. Anaripoti Mwandishi Wetu.

Naibu Waziri huyo Viktor Gulevich ambaye pia ni Meja Jenerali ameandika barua ya kujiuzulu jana tarehe 6 Machi, 2022 na kuiwasilisha kwa bosi wake yaani Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo, Viktor Khrenin.

Meja Jenerali Gulevich alisema kwamba baadhi ya wanajeshi wa Belarusi walikataa kushiriki katika vita ya Urusi na Ukraine hii ikiwa ni baada ya kupata shinikizo kutoka katika Serikali ya Belarusi kwa sababu tu nchi hiyo ina uhusiano wa karibu na Urusi.

Pamoja na hatua hiyo aliyochukua, Naibu Waziri huyo ni moja ya maofisa wa Serikali ya Belarusi ambaye amewekewa vikwazo na Serikali ya Uingereza kutokana na ukaribu wao na Putin.

Licha ya kusimamia mazoezi ya kijeshi ambayo ni maandalizi ya vikosi vya Jeshi la Belarusi kuungana na wanajeshi wa Urusi, uamuzi wake wa kujiuzulu unakuwa pigo kwa Putin kwani utachochea viongozi wengine wakubwa nchini humo kupinga uamuzi wa Putin kuivamia Ukraine.

1 Comment

  • Asante mwandishi aliyejiuzuru ni mtu sio serekali pigo liko wapi kwa Putin .mtu kujiuzuru au kufukuzwa kazi ni jambo la kawaida katika ulimwengu wa kazi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!