Wednesday , 22 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Mbowe: ACT-Wazalendo wataka sheria kumdhibiti DPP, DCI
Habari za Siasa

Kesi ya Mbowe: ACT-Wazalendo wataka sheria kumdhibiti DPP, DCI

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeshauri mifumo ya utawala na utoaji haki jinai nchini iboreshwe, ili kukomesha changamoto ya watu kubambikiwa kesi za kisiasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumatatu, tarehe 7 Machi 2022 na Msemaji wa Kisekta wa Mambo ya Ndani wa ACT-Wazalendo, Mabarala Maharagande.

Akizungumzia hatua ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu, kumfutia mashtaka ya ugaidi Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, kwenye Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, jijini Dar es Salaam.

“Mbowe hakushinda kesi, tupiganie kupatikana kwa mifumo imara ya uongozi wa nchi na utoaji haki. Mhimili wa mahakama uwe huru kuendesha masuala yake, siasa isiamue juu ya upatikanaji haki,” imesema taarifa ya Maharagande.

Taarifa ya Maharagande imesema, zinahitajika sheria zitakazodhibiti mamlaka ya ofisi ya DPP na Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), ili panapotokea uzembe wa kiutendaji katika ofisi hizo, wahusika wawajibike kisheria.

“Pawepo na sheria zinazoweka udhibiti wa mamlaka na ofisi ya DPP na watendaji wake, ili pale panapotokea uzembe, nia ovu pawepo na uwajibikaji kisheria. Mamlaka ya DCI na upelelezi wa kesi yaboreshwe na pawepo ukomo wa upelelezi wa kesi za aina hii zisizokuwa na dhamana,” imesema taarifa ya Maharagande.

Taarifa hiyo imesema “ kianzishwe chombo huru cha kuchunguza Jeshi la Polisi (Independence Police Oversight body) ili ichunguzwe vitendo vyote vya utovu wa maadili na makosa yanayoweza kuathiri haki za wananchi.”

Katika hatua nyingine, Maharagande kuitia taarifa hiyo, imeshauri mahakama ziwe na mamlaka ya kusikiliza maombi ya dhamana kwa makosa yasiyokuwa na dhamana, ili kupeuka kuwaumiza watuhumiwa.

“Zoezi la kuwaachia Watanzania wenzetu waliomaarufu na wasio na umaarufu liendelezwe ili kila raia awe na haki ya kunufaika na Uhuru wa nchi yake na matakwa ya kikatiba,” imesema taarifa ya Maharagande.

Mbowe na wenzake waliokuwa makomando wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Hlafan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillha Ling’wenya, waliachwa huru na mahakama hiyo.

Baada ya DPP Sylvester kupitia Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando, kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka ya ugaidi yaliyokuwa yanawakabili.

Mbowe na wenzake walikuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 16/2021, iliyokuwa na mashtaka matano ya ugaidi, likiwemo la kupanga kudhuru viongozi wa Serikali, kupanga maandamano yasiyo na kikomo, kulipua vituo vya mafuta na maeneo yenye mikusanyiko ya watu.

Walidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mei hadi Agosti 2020, kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Kilimanjaro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yanawa mikono fidia Kimara-Kibamba

Spread the loveSERIKALI imewataka waathiriwa wa bomoabomoa ya upanuzi wa barabara ya...

Habari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

Habari za SiasaKimataifa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Habari za Siasa

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla...

error: Content is protected !!