Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Prof. Muhongo akagua ujenzi miradi ya maji
Habari Mchanganyiko

Prof. Muhongo akagua ujenzi miradi ya maji

Spread the love

MBUNGE wa Musoma Vijijini, mkoani Mara, Prof. Sospeter Muhongo, amefanya ziara ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali jimboni humo.Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara…(endelea).

Prof. Muhongo amefanya ukaguzi huo hivi karibuni, akiambatana na Kamati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Miongoni mwa miradi inayotekelezwa jimboni humo na Mamlaka ya Maji ya RUWASA, ni mradi wa maji wa kata ya Bwasi, kutoka chanzo Cha Ziwa Victoria, unaotarajiwa kukamilika kabla ya tarehe 30 Oktoba 2023.

“Vijiji vitakavyonufaika na upatikanaji wa maji ya bomba ya mradi huu ni Bwasi, Bugunda na Kome, ambapo ujenzi wa tenki la maji la ujazo wa Lita 150,000 unakamilishwa. Gharama za mradi huu ni Sh. 997.7 milioni,” imesema taarifa ya Ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini.

Mradi mwingine unaoendelea kutekelezwa jimboni humo ni, mradi wa Chumwi-Mabuimerafuru, ukihusisha ujenzi wa tenki la ujazo wa Lita 300,000 na  vituo vya kuchotea maji 17.

Mradi huo unagharimu Sh. 1.6 bilioni, ulianza kutekelezwa Februari 2023 na unatarajiwa kukamilika kabla ya tarehe 30 Oktoba mwaka huu.

“Wananchi wa Musoma Vijijini na viongozi wao wa ngazi zote wanaishukuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuendeleza kutupatua fedha za utekelezaji miradi yetu ya Maendeleo,” imesema taarifa hiyo.

Katika ziara hiyo, wananchi wa Musoma Vijijini, waliwasilisha kero zao kwa Prof. Muhongo, ambazo zilipatiwa majibu.

Musoma Vijijini ina kata 21, zenye vitongoji 374, ambavyo vyote vina miradi ya maji ambayo Iko katika hatua mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!