Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Prof. Mbarawa atoa maagizo kwa bodi ya ushauri ya TBA
Habari Mchanganyiko

Prof. Mbarawa atoa maagizo kwa bodi ya ushauri ya TBA

Spread the love

 

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa ameitaka Bodi Mpya ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kuuwezesha Wakala huo kuwekeza kikamilifu katika viwanja vyake vilivyopo katika maeneo ya kimkakati ili kumaliza tatizo la upungufu wa nyumba za viongozi na watumishi wa umma lililopo nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza mara baada ya kuzindua Bodi hiyo jijini Dar es Salaam, Prof. Mbarawa amesema huu ndio wakati wa TBA kujiimarisha kimiundombinu na kiuchumi kwa kutumia fursa ya mahitaji ya nyumba kwa ajili ya watumishi wa umma na majengo ya kibiashara katika miji mikuu.

“..Hakikisheni mnakuja na mipango ya kutumia rasilimali ya viwanja na majengo mlio nayo kupata faida kwa kujenga majengo mazuri katika maeneo ya miji na kuhakikisha nyumba zenu zaidi ya elfu sita zilizopo zinakuwa katika viwango bora wakati wote na kuvutia wapangaji,” amesema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa ameipongeza TBA, kwa mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi 3,500 Nzuguni Jijini Dodoma na kuongeza kuwa mradi huo ukikamilika kwa wakati utawaongezea mapato kwa kuwa bado mahitaji ya nyumba za viongozi na watumishi wa umma katika maeneo ya mijini ni makubwa.

“…Tengenezeni mikakati ya ubunifu itakayo wawezesha kushirikiana na sekta binafsi ili kuhakikisha sekta ya majenzi na makazi ya viongozi na watumishi wa umma inaimarika,” amesisitiza Prof. Mbarawa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TBA, Dk. Ombeni Swai amesema Bodi yake itafanya kazi kwa uadilifu na ubunifu ili kuiwezesha TBA kupata faida na kutoa huduma ya kuaminika kwa Watanzania.

Naye Mtendaji Mkuu wa TBA, Daud Kondoro amemshukuru Waziri Prof. Mbarawa kwa miongozo anayoitoa na kusisitiza kuwa TBA itaendelea kusimamia mifumo, nidhamu, udhibiti na uendelezaji wa miradi mbalimbali ya nyumba na majengo ya Serikali nchini kote kwa kuzingatia mahitaji na faida ili kukuza mtaji ikiwemo ujenzi wa nyumba 3,500 jijini Dodoma.

Wajumbe wapya wa Bodi ya Ushauri ya TBA itakayohudumu kwa miaka mitatu ni pamoja na Dk. Ombeni Swai (Mwenyekiti), Optatus Kanyesi (Mjumbe), Shaban Kabunga (Mjumbe), Joseph Mkali (Mjumbe), na Vicky Jengo (Mjumbe).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!