Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bilioni 2/- kuboresha kilimo cha pamba
Habari Mchanganyiko

Bilioni 2/- kuboresha kilimo cha pamba

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imesaini mkataba wa zaidi ya Sh 2.1 bilioni na nchi ya Brazili kwa ajili ya uboreshaji wa sekta ya kilimo bora cha zao la pamba nchini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea)

Utiaji saini mradi huo umewashirikisha Balozi wa Brazil nchini Tanzania Antonio Agustors Martin Cesar, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Brian Bogart na wadau wengine.

Mradi huo uliosainiwa jana Jumatano tarehe 20, Julai, 2022, umelenga kuongeza thamani katika zao la pamba ujulikanao kama ‘Beyond Cotton Project’

Mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi 20 na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Bodi ya Pamba (TCB) pamoja na Wizara ya Kilimo.

Baada ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba huo Balozi Cesar, Kaimu Mkurugenzi WFP, Bogart, Gunga Mbavu ambaye alimwakilisha mgeni rasmi ambaye ni katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo na Mkurugenzi TCB, Marco Mtunga wamesema kuwa kilimo bora cha pamba kitaimarisha uchumi wa Watanzania na wakulima kwa ujumla.

Kwa nyakati tofauti viongozi hao wameeleza kuwa mikataba ya uboreshaji wa kilimo cha pamba nchini kitaongeza ufanisi wa kipato cha wakulima wa zao hilo pamoja uchumi wa taifa kwa ujumla.

Balozi Cesar amesema Brazil wataendelea kushirikiana na nchi ya Tanzania kwa kuimarisha kilimo cha pamba nchini ili kuwa na tija katika zao hilo.

Amesema mradi wa kusaidia utafiti wa usalama chakula na lishe na kuongeza thamani ya zao la pamba utahusisha kaya 8,800 sawa na asiliia 50 vijana watakaonufaika.

Aidha ameeleza kuwa kwa mwaka 2030 kilimo kitakuwa kina uwezo wa kuzalisha asilimia 10 ya pato la taifa.

Naye Mkurugenzi TCB, Mtunga amesema pamba ni zao ambalo litaongeza tija kwa mkulima pamoja vijana kuweza kujikwamua kimaisha.

Katika hatua nyingine alisema mkataba wa kilimo bora cha pamba ni kuendeleza zao hilo na utafiti wa mbegu bora zisizoshambuliwa na wadudu na magonjwa kama ilivyokuwa hapo awali.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dk.Geofrey Mkamilo amesema taasisi hiyo itaendelea kufanya utafiti wa mbegu bora ambazo zitaongeza tija kwa wakulima wapamba.

Aidha, amesema mradi wa kilimo cha pamba utatekelezwa katika mkoa wa Mwanza katika Wilaya ya Magu, Misungwi na Kwimba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Habari Mchanganyiko

Makonda autaka mgodi kubadilisha maisha ya wana-Geita

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ametoa wito kwa...

error: Content is protected !!