August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia mgeni rasmi siku ya mashujaa

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani anatarajiwa kuwa ngeni rasmi katika sherehe za kumbukumbu ya mashujaa itakayofanyika kitaifa jijini Dodoma katika viwanja vya Mashujaa tarehe 25 Julai mwaka huu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Katika maadhimisho hayo mkuu wa Mkoa Anthony Mtaka ataongoza kuwasha mwenge wa mashujaa tarehe 24 saa sita kamili usiku na tarehe 25 saa sita kamili usiku Meya wa jiji la Dodoma Prof.Davis Mwanfupe ataongoza kuuzima mwenge wa mashujaa.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi tarehe 21, Julai, 2022, na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka alipokuwa akikagua maandalizi ya shughuli hizo ambayo yanaendelea kufanyika katika viwanja hivyo.

Mtaka amesema kuwa Rais Samia ametoa heshima hiyo ya kufanyika sherehe hizo Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kuendelea kuukuza mkoa wa Dodoma kama sehemu ya makao makuu ya nchi.

Akizungumzia na kamati ya Mkoa na pamoja na kamati ya maandalizi ya kitaifa, Mtaka amesema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri tayari kwa ajili ya kilele hicho.

Sambamba na hayo Mtaka amesema ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Wilaya ,Jiji na Kurugenzi ya maadhimisho ya taifa Ofisi ya Waziri Mkuu wataangalia namna ya kuboresha uwanja wa Mashujaa ili iwe alama ya jiji la Dodoma na kutoa fursa kuwa sehemu ya kivutio katikati ya jiji hilo.

Aidha amesema kuwa changamoto zilizotolewa za ukarabati na mwenge, Mtaka amesema kuwa changamoto hizo haziwezi kujirudia tena katika maadhimisho mengine.

Pamoja na hayo, amewataka wananchi wa Mkoa wa Dodoma pamoja na watu wengine kutoka mikoa ya jirani kuhakikisha wanahudhuria madhimisho ya siku hiyo na wajasiriamali kutumia fursa hiyo kujiingizia kipato.

error: Content is protected !!