Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba amgeuka Jaji Mutungi
Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba amgeuka Jaji Mutungi

Spread the love

MTAFARUKU mkubwa umeibuka ndani ya Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, kufuatia mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohammed Nchengerwa, kuamuru pande mbili zinazopingana ndani ya Chama cha Wananchi (CUF), kugawana muda wa kutoa maoni ndani ya kamati hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Katiba na Sheria zinaeleza kuwa mara baada ya Nchengerwa kuelekeza kuwa kila upande kati ya Prof. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti anayetambuliwa na msajili wa vyama na Maalim Seif Shariff Hamad, katibu mkuu wa chama hicho anayetambuliwa na wanachama wa chama hicho.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mgogoro huo ulipamba moto kufuatia baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, kushinikiza mwenyekiti kutoa dakika 30 kwa kila upande. Nchengerwa aligomea pendekezo hilo.

Akizungumza ndani ya kamati ya katiba na sheria, Prof. Lipumba alisema, msajili wa vyama hana nguvu ya kukikaba Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuliko anavyoweza kuvikaba vyama vya upinzani.

Alisema,“…huyu msajili wa vyama vya siasa, ni mteule wa rais ambaye ni mwenyekiti wa chama kilichoko madarakani. Hivyo kwa vyovyote vile, anaweza kuvibana vyama vya upinzani kuliko anavyoweza kukishughulikia chama tawala.”

Alipoulizwa kuhusu nafasi ya msajili wa vyama vya siasa, katika kutatua migogoro ya ndani ya vyama hivyo, Prof. Lipumba alisema, “uwezo huo ni mdogo sana.” Alisema, migogoro ndani ya vyama, inapaswa kutatuliwa ndani ya vyama vyenyewe.

Aidha, Prof. Lipumba alidai kuwa vifungu vinavyotoa mamlaka kwa msajili wa vyama kutoa taarifa kuhusu mafunzo ya ndani ya vyama hivyo, haviwezi kutekelezeka kwa kuwa ofisi hiyo haina uwezo wa kufanya kazi hiyo.

Naye Joram Bashange, kaimu katibu mkuu wa CUF Tanzania Bara, ameiambia kamati ya katiba na sheria, kwamba muswaada uliopo ndani ya Bunge, ni mgumu kwa vyama hivyo kufanya kazi zake kama inavyotakiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!