Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Viongozi wa Dini wapewa somo
Habari Mchanganyiko

Viongozi wa Dini wapewa somo

Spread the love

ASKOFU wa Jimbo la Dodoma kanisa la Mlima wa Moto,Silvanusi Komba amewataka viongozi wadini kuhakikisha wanawafundisha waumini wao juu ya kufanya  kazi kwa bidii badala ya kufundisha masomo ya utoaji tu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akihubiri katika ibada ya Jumapili askofu Komba alisema mwaka 2019 ni Mwaka pekee wa watanzania kutambua umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii badala ya kukaa vijiweni na kuilalamikia serikali. 

Kiongozi huyo wa Kiroho alisema kuwa apendezwi kuona waumini wa kanisani lake kuendelea kulalamika kwa madai kuwa maisha ni magumu.

Akiwahutubia maelfu ya waumini kanisani hapo alisema kuwa dhambi kubwa inayofanywa na viongozi wengi ni kushindwa kuwafundisha waumini wao kufanya kazi kwa bidii.

“Hakuna mtu ambaye anaweza kukuona katika dimbwi la umasikini kama mtu hata weza kufanya kazi kwa bidii na juhudi kubwa na kwa ustadi wa kazi.

“Hakuna serikali yoyote duniani ambayo anaweza kufanya uchumi wa mtu mmoja mmoja kwa kukuletea fedha au mahitaji bali kupitia katika kazi ambazo unazozifanya.

“Nashangaa kuona baadhi ya watu ambao wanataka kubarikiwa bila kufanya kazi yoyote,unategemea utapataji maendeleo bila kufanya kazi?”alihojo Askofu Komba.

Katika hatua nyingine amisema katika mwaka wa 2019 ni Mwaka wa mafanikio kwa wale ambao wanafanya kazi kwa bidii na kutambua kuwa mwaka huu siyo mwaka wa uendeleo.

Kiongozi huyo alisema watu wengi wana lala mikakati kuwa maisha ni magumu kwa kushindwa kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi jambo ambalo ni dalili za umasikini.

“Wapo watu ambao wamemaliza vyuo vikuu lakini kutokana na uzembe na uvivu wamekuwa wakitembea na vyeti wakitafuta ajira badala ya kutumia elimu yao kufanya kazi za kujiajiri,” alisema Askofu Komba.

Aidha alisema anasifia utendaji wa serikali ya awamu ya tano kwa kupambana na Rushwa pamoja na masuala ya uonevu na badala yake kwa sasa kila mmoja anafanya kazi kwa uaminifu.

“Nataka niwaambie waumini wangu hata kama mtalala kanisani kwa kuomba mafanikio lakini kama hakuna juhudi ya kufanya kazi hakuna baraka ambazo zinaweza kuwa juu yako.

“Fuatilia hotuba za Rais Magufuli amekuwa akihamasisha kufanya kazi,si kwamba yeye ndiye mwanzilishi wa kuhamasisha kufanya kazi bali ni maagizo ya Mumgu kuwataka watu kufanya kazi.

“Katika maandiko matakatifu yanaeleza kuwa mtu asiyefanya kazi na asile lakini inaend mbali zaidi kuwa utabarikiwa mashambani na mjini na muingiapo na mtokapo kwa maana nyingine ni lazima ufanye kazi”alieleza Askofu Komba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!