Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Prof. Kakoko: Chanjo UVIKO-19 haisababishi ugumba, upungufu nguvu za kiume
Afya

Prof. Kakoko: Chanjo UVIKO-19 haisababishi ugumba, upungufu nguvu za kiume

Spread the love

 

MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Profesa Deodatus Kakoko, ametoa wito kwa wananchi kuchanjwa chanjo ya Ugonjwa wa Corona (UVIKO-19), kwani haina madhara kama inavyodaiwa na baadhi ya watu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Prof. Kakoko ametoa wito huo leo Jumamosi, tarehe 27 Novemba 2021, akitoa mada katika semina ya wanahabari kuhusu afua za kinga dhidi ya tishi la wimbi la nne la UVIKO-19 na chanjo ya ugonjwa huo.

Iliyoandaliwa na Shirika linaloshughulika na masuala ya afya, Amref Health Africa Tanzania.

Prof. Kakoko amesema dhana inayodai kwamba chanjo hizo zinaathiri afya ya uzazi wa mwanamke na kusababisha tatizo la ugumba pamoja na kupunguza nguvu za kiume, si ya kweli.

“Lakini dhana juu afya ya uzazi na nafikiri liligusa pabaya kila mmoja anavyojua, sababu mara nyingi wote akili zetu ziko huko lazima tuwe na uhakika, imani imelezwa kuwa chanjo inaathiri uzazi wa wanawake wasizae, wawe wagumba na inaathiri nguvu za kiume,” amesema Prof. Kakoko.

Prof. Kakoko amesema “watu wengi wamekuwa wakikwepa lakini maneno hayo si kweli, uchunguzi wa kisayansi umeonesha hakuna kitakachochangia kupunguza nguvu za kiume na waelimishaji tumeenda kueleza jamii.”

Vile vile, Prof. Kakoko amewashauri wananchi waepukane na dhana potofu ya kwamba UVIKO-19 unawaathiri matajiri, wazee na watu waishio maeneo ya mjini peke yake, kwani siyo ya kweli kwa kuwa janga hilo linawathiri watu wote.

Mhadhiri huyo wa MUHAS amesema chanjo zilizoingiwa nchini zimefanyiwa uchunguzi na taasisi za Serikali, na kubainika kutokuwa na madhara.

Prof. Kakoko ametaja taasisi zilizofanya uchunguzi huo, ikiwemo Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Taasisi ya Taifa ya Utaiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini (NIMR) na vyuo vikuu kadhaa.

“Sisi tulijihakikishia tunaziangalia, tunazikagua kuona kama zinafaa, kila chanjo hukagulwia taasisi  za Serikali. Wamefanya kazi kubwa na taasisi zote zimechunguza, hii inatupa uhakika dhana hizi hazina ukweli wowote,” amesema Prof. Kakoko.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!