January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kirusi kipya tishio, mataifa yazuia ndege kutoka Kusini mwa Afrika

Spread the love

MATAIFA mbalimbali duniani ikiwemo Ufaransa yameanza kuzuia safari za ndege kutoka mataifa ya Kusini mwa bara la Afrika, baada ya aina mpya ya kirusi cha Covid 19 kilichopewa jina la B.1.1.529 kugunduliwa mapema wiki hii. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Aidha, kirusi hicho tayari kimepenya hadi nchi ya Ubelgiji iliyopo barani Ulaya ambapo kwa imeripoti kisa cha kwanza cha kirusi hicho.

Ufaransa imesema inasitisha safari hizo kwa kipindi cha saa 48 zijazo, huku Mkuu wa Tume ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen akipendekeza hatua zaidi kuchukuliwa kuhusu safari za ndege kutoka Kusini mwa Afrika.

Uingereza nayo imechukua hatua kama hiyo, na kusitisha safri za ndege kutoka mataifa ya Afrika Kusini, Lesotho, Botswana, Zimbabwe, Msumbiji, Namibia na Eswatini.

Kenya nayo imetangaza kuwa abiria kutoka mataifa hayo, watawekwa karatini na kufanyiwa vipimo mara kadhaa kabla ya kuruhusiwa kutangamana na watu nchini humo.

Wanasayansi wanasema wanaendelea kufanya utafiti zaidi kuhusu kirusi hiki kipya, ambacho kinaonekana kuzua wasiwasi mkubwa, huku biashara katika masoko ya hisa duniani, ikiyumba.

Shirika la Afya Duniani (WHO) wanakutana kujadilli aina hii mpya ya kirusi na kukipa jina la Kigiriki kama lilivyo kwa kirusi cha Alpha na Delta.

Mpaka sasa, Shirika la afya duniani linasema hata hivyo ni visa chini ya 100 ya kirusi hiki kipya ndivyo vilivyoripotiwa katika mkoa wa Gauteng nchini Afrika Kusini, visa vinne nchini Botswana na kimoja huko Hong Kong.

Hii inajiri wakati huu Afrika Kusini, asilimia 24 ya watu wake wakiwa wamepokea chanjo kamili ya kupambana na Covod-19, na kuna hofu kuwa, huenda kirusi hiki kipya kikasambaa kwa kasi.

error: Content is protected !!