Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Prof. Kabudi afuturisha waumini wa dini y kiislam Kilosa, asisitiza amani
Habari Mchanganyiko

Prof. Kabudi afuturisha waumini wa dini y kiislam Kilosa, asisitiza amani

Spread the love

 

MBUNGE wa Jimbo la Kilosa Prof. Palamagamba Kabudi amewataka waumini wa dini kiislam na dini nyingine katika madhehebu tofauti wilayani Kilosa kulinda misingi ya amani iliyoasisiwa na waasisi wa Taifa la Tanzania kwa kuwataka wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi katika shughuli zao ili kuendelea kujenga Uchumi imara wa Taifa. Anaripoti Yusuph Kayanda, Morogoro … (endelea).

Akizungumza na mamia ya waumini wa dini ya kiislam wilayani Kilosa walioungana pamoja kushiriki katika Iftar iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Prof. Palamagamba Kabudi katika msikiti wa Rudewa na kuhudhuliwa na viongozi wa dini mbalimbali akiwemo Shekh Mkuu wa Wilaya Sheikh Nassoro Milambo, amesema misingi ya amani ikiendelea kuasisiwa vyema itajenga jamii bora yenye upendo na kulitumikia Taifa kwa uzalendo.

Prof. Kabudi aliendelea kuwasisitizia waumini wa dini ya Kiislam kuwa Maisha waliokuwa wakiishi katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uliowajenga waumini hao katika mioyo yenye upendo na kuoneana huruma kwa kufturu pamoja, kufanya ibada pamoja ndio Maisha sahihi yenye kukuza Taifa lenye amani, kuheshimiana kwa dini zote ndio misingi itakayowajenga vijana kuwa wazalendo.

Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Prof. Palamagamba Kabudi

Aidha alitumia jukwaa hilo kuwaeleza wananchi juu ya neema kubwa na baraka za Mwenyezi Mungu kwa kuwanusuru wakazi wa Rudewa na janga la mafuriko yaliyotokea Wilayani humo na kuwasihi waendelee kushika Imani za dini ndio ponyo katika Mioyo ya Wanadamu.

Awali akimkaribisha Mbunge huyo, Sheikh Mkuu wa Wilaya Kilosa, Shekh Nassoro Milambo amepongeza jitihada kubwa zilizofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananchi wa Kilosa Maendeleo makubwa ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya Barabara, Shule mpya za Sekondari pamoja uboreshaji wa miundombinu ya Mawasiliano.

Sheikh Milambo alisema Maendeleo hayo makubwa kamwe hayajawahi kutokea na kukiri kuwa yanatokana na kumpata Mbunge mwenye kufanya kazi kwa weledi na upendo kwa wananchi wake kwa kuendelea kuchechemua shughuli za kimaendeleo Wilayani humo.

Sheikh Mkuu wa Wilaya Kilosa, Shekh Nassoro Milambo

Aidha katika Iftari hiyo Waumini wa dini ya Kiislamu wakiongozwa na Shekh Mkuu wa Wilaya walitumia Fursa hiyo katika kufanya Dua maalumu kwa kuliombea Taifa na Kumuombea Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliongoza Taifa vyema pamoja na kumtakia Heri Mbunge wao kusimamia vyema Miradi inayotekelezwa jimboni humo itakayosaidia kuchagiza Uchumi kwa Wananchi na Taifa kwa Ujumla.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!