Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Kiruswa aagiza menejimenti kutatua changamoto za wafanyakazi wizara ya madini
Habari Mchanganyiko

Dk. Kiruswa aagiza menejimenti kutatua changamoto za wafanyakazi wizara ya madini

Spread the love

Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa ametoa rai kwa menejimenti ya wizara ya madini kuhakikisha inachukua hatua za dhati katika kutatua changamoto ambazo zinawakabili watumishi wa wizara na kuzifanyia kazi ili kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu yao. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Alitoa rai hiyo tarehe 8 Aprili 2024, wakati akifunga Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Madini lililofanyika Mji wa Serikali Mtumba – Jijini Dodoma.

Dk. Kiruswa alisema ni muhimu menejimenti kukumbuka mara zote kuwa watumishi ndiyo hazina kuu ya kutekeleza, kusimamia na kuhakikisha malengo yaliyowekwa ya wizara na sekta ya madini yanatimia.

“Ni vyema tukaijali hazina hiyo. Aidha, ni vema kwa menejimenti ya wizara kuchukua hatua katika kutatua changamoto ambazo zinalalamikiwa na Watumishi wa Wizara na kuzifanyia kazi.

“Ni matumaini yangu kuwa mtazingatia yale mliyoyapata katika mkutano huu na nisisitize suala la uwajibikaji na uzingatiaji wa sheria na kanuni katika utekelezaji wa majukumu yetu” amesema Dk. Kiruswa.

Pia Dk. Kiruswa alisistiza kuhusu kutekeleza maelekezo aliyoyatoa Waziri wa Madini, Anthony Mavunde wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo ili kuwezesha maendeleo ya sekta.

Awali, Waziri Mavunde alisisitiza kuongeza ubunifu na kwamba milango yake iko wazi kwa watumishi kumshauri kwa manufaa ya wizara na sekta ya madini.

Kwa upande wake, Mweyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Madini na Naibu Katibu Mkuu, Msafiri Mbibo alisema kuwa wizara itaendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi huku akiahidi kuwa menejimenti itafanyia kazi maelekezo ya waziri kuhusu kusikiliza na kutatua changamoto za wafanyakazi sambamba na kuendelea kuwajengea uwezo ili kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!