RAIS wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Profesa Edward Hoseah, amewataka mawakili wapya, kuwasaidia wananchi katika kutatua migogoro inayowakabili.Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).
Prof. Hoseah ametoa wito huo leo Ijumaa, tarehe 8 Julai 2022, jijini Dar es Salaam, katika hafla ya kuwakubali na kuwapokea mawakili wapya 335.
“Tuna kanda 21, ningependa nitumie wasaa huu mtakapotawanyika tukumbuke kurudisha fadhila kwa Watanzania, na kurudisha fadhila ni kutatua migogoro. Mwaka huu tunajikita sehemu zote za kanda na makao makuu ya TLS, kwamba msaada wa kisheria kwa Watanzania wote tuutoe maana ni wajibu na jukumu letu,” amesema Prof. Hoseah.
Aidha, Prof. Hoseah amewataka mawakili hao kufuata maadili yao ya taaluma yao ya sheria pamoja na kutumia mihuri ya kielektroniki ili kutokomeza changamoto ya mawakili vishoka..”
Leave a comment