NAIBU Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Evaristo Longopa, amewataka mawakili kutokuwa chanzo cha kukwamisha uendeshaji mashauri, ili haki itendeke kwa wakati. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).
Dk. Longopa ametoa maagizo hayo leo Ijumaa, tarehe 8 Julai 2022, katika hafla ya kukukubali kuwapokea mawakili wapya zaidi ya 300, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
“Ndugu zangu mawakili ninyi mnapaswa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu na mhakikishe kwamba haki inatendekea, msiwe chanzo cha kusababisha mashauri kutokamilika kwa kuomba maahirisho yasiyokuwa na sababu ili haki ipatikane kwa wakati,” amesema Dk. Longopa na kuongeza:
“Na msiicheleweshe haki, nawatakia majumu mema naamini mtakuwa mawakili wema na wenye maadili ili tasnia yetu ya sheria iendelee kuheshimika.”
Leave a comment