JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, amewataka mawakili wapya na wale wa zamani ambao hawana ajira, kujikita katika masuala ya usuluhishi kwani ndiko fursa hizo zinapatikana katika nyakati hizi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).
Akizungumza katika hafla ya kukubali kuwapokea mawakili wapya 335, leo Ijumaa, jijini Dar es Salaam, Prof. Juma amewaeleza kuwa, wateja wengi hawaendi kupata huduma za kimahakama kwa kuwa kesi zinachukua muda mrefu, hivyo wamehamia katika masuala ya usuluhishi.
“Siku hizi wateja wengi wanapatikana katika maeneo ya usuluhishi na wengi hawaendi kupata huduma katika kesi za mahakamani sababu zinachukua muda mrefu. Taratibu za kimahakama ni nyingi sana,” amesema Prof. Juma.
Prof. Juma amesema “kwa hiyo kwenye usuluhishi ni lazima kujikita sababu ni eneo linalokuwa na wananchi wengi hasa sekta binafsi wanapenda. Ajira imehama kutoka kuendesha mashauri mahakamani na kuhamia katika usuluhishi na majadiliano.”
Katika hatua nyingine, Prof. Juma ame Baraza la Shule ya Sheria na Shule ya Sheria kwa Vitendo, kushirikiana na vyuo vikuu katika kufanya mabadiliko ya mitaala ili ipatikane itakayosaidia wanafunzi kuajiriwa na kujiajiri katika soko la ajira la sasa.
“Hali ya nchi imebadilika sana na dunia imebadilika, sisi tunahitaji kubadilika. Kwa hiyo tunahitaji mabadiliko kwenye mitaala hasa ya shule ya sheria kwa vitendo.
Inabidi tubadilishe mitaala sio tu itawajenga katika kufanya kazi za kisheria lakini lazima iwajenge kuishi na kufanya kazi katika dunia inayotegemea teknolojia,” amesema Prof. Juma.
Leave a comment