September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Polisi washambulia gereza, wamtorosha kamanda wao aliyekamatwa

Spread the love

 

POLISI wa kupambana na ugaidi nchini Mali wamelalamikiwa baada ya maofisa wenye silaha kuandamana kwenda gerezani kushinikiza kamanda wao aachiliwe huru. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea). 

Aidha, taarifa kutoka nchini humo zinasema kuwa walinzi wa gereza waliondoka, wakati nyingine zinasema serikali iliamuru aachiliwe kuepusha machafuko.

Kamanda Oumar Samake alishtakiwa kwa mauaji juu ya vifo vya waandamanaji wapatao 14 wanaopinga serikali Julai 2020.

Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa Serikali ya mpito ya Mali ililaani kitendo hicho cha “watu waliovalia sare na wenye silaha” kutoka Kikosi Maalum cha Kupambana na Ugaidi (Forsat).

Chama cha Haki za Binadamu cha Mali (AMDH) kimesema shambulio hilo ni kama shambulizi dhidi ya sheria.

Ilisema maofisa walikuwa wamefyatua risasi katikati mwa mji mkuu, Bamako, Ijumaa tarehe 3 Septemba kabla ya kuelekea kwenye gereza kuu la jiji, ambapo kamanda wa Samake alikuwa amezuiliwa kwa saa kadhaa mapema.

Kitengo hicho cha vikosi maalum kimepokea mafunzo kutoka kwa EU na Marekani kusaidia katika vita dhidi ya vikundi vya jihadi ambavyo vimekuwa vikifanya uasi kwa muda wa miaka kumi nchini Mali.

UN na Ufaransa zina maelfu ya walinda amani walioko huko kusaidia kukabiliana na wanajihadi.

Hata hivyo, machafuko hayo yameiacha nchi hiyo bila utulivu huku kukishuhudiwa mapinduzi mawili ya kijeshi mwaka 2020.

error: Content is protected !!