Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo Mahaba ya Nandy, Billnass usipime…mashabiki walipuka
Michezo

Mahaba ya Nandy, Billnass usipime…mashabiki walipuka

Spread the love

 

NANI alikuambia wameachana? Hawajaachana ng’o! ndivyo walivyowathibitishia mashabiki wao wasanii wa Bongofleva, Faustina Mfinanga ‘Nandy’ na William Lyimo ‘Billnass’ waliposhusha shoo kali katika kilele cha tamasha la ‘Nandy Festival’ jijini Dar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Wawili hao ambao kwa tangu Februari hawajaonekana hadharani pamoja, waliwafurahisha mashabiki baada ya kuperfom pamoja jana tarehe 4 Septemba 2021 katika shoo hiyo iliyopigwa katika viwanja vya Posta Kijitonyama.

Mauno ya Nandy, pamoja na mahaba murua ndiyo yaliyoinua shangwe za mashabiki hao ambao walipigia mstari kuwa couple hiyo imerudi upya.

Aidha, baada ya shoo hiyo, Billnass alimpa mashavu ya kutosha Nandy mbele ya waandishi wa habari kwa kueleza kuwa ni mwanamke imara ambaye ni mfano wa kuigwa kwa mabinti wanaotaka kuwa kama yeye kwenye kiwanda cha muziki.

“Kuhusu kufanya shoo pamoja ni kwamba watu wamekuwa wakipenda tupande jukwani pamoja ila bahati mbaya ratiba zangu zikawa zinanibana ila leo (jana) imewezekana kwa sababu naheshimu vitu anavyofanya… hii ni shoo, haihusiani na mapenzi,” alijidai Billnass.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!