Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mapinduzi Guinea: Rais akamatwa na waasi
KimataifaTangulizi

Mapinduzi Guinea: Rais akamatwa na waasi

Alpha Condé, Rais wa Jamhuri ya Guinea
Spread the love

 

ALPHA Condé, Rais wa Jamhuri ya Guinea, amekamatwa na jeshi linalodai limechukua madaraka ya kuongoza taifa hilo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Tayari Umoja wa Afrika (AU), umelaani mapinduzi hayo na kulitaka jeshi kumuachilia rais Conde mara moja.

Katika taarifa yake kwa umma, rais wa AU Felix Tshisekedi na rais wa tume ya AU Moussa Faki, wameitisha mkutano wa dharura wa taasisi za umoja huo kuhusu usalama na amani ili kutathmini hali nchini Guinea.

Mkutano huo unalenga pia kuchukua hatua zinazoweza kusaidia kurejesha utulivu nchini humo.

Jana Jumapili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Gutteres, alituma ujumbe kwa njia ya twitter, akijibu kinachotokea Guinea.

Alisema, anafuatilia hali hiyo kwa karibu na kulani kuchukuliwa serikali kwa nguvu ya bunduki. Ametaka  kuachiliwa mara moja rais Conde.

Mpaka sasa, hakuna anayefahamu hatima ya rais Condé, kufuatia video ambayo haijathibitishwa kumuonyesha akiwa mikononi mwa wanajeshi, ambao walisema wamefanya mapinduzi.

Hata hivyo, waziri wa ulinzi amenukuliwa akisema, jaribio hilo la kuichukua serikali lilikuwa limeshindwa.

Hii inafuatia saa kadha za makabiliano ya risasi karibu na Ikulu ya rais, katika mji mkuu, Conakry.

Jeshi ambalo limedai kuchukua madaraka nchini humo, limetangaza kwamba litafanya mkutano leo na mawaziri na wakuu wa taasisi zilizovunjwa jana mjini Conakry.

Aidha, wanajeshi hao wametangaza amri ya kutotoka nje kuanzia saa mbili usiku.

Bado haifahahamisja ni nini kinatokea Conakry, lakini wanajeshi wanasema, wamechukua udhibiti. Katika hotuba iliyoonyeshwa kwa njia ya televisheni, wanaume walio na sare za kijeshi, bendera ya Guinea ikiwa nyuma yao wamelihutubia taifa na kutangaza kumuondoa rais.

Wakijiita Kamati ya Kitaifa ya upatanisho na maendeleo, wanalaumu ufisadi uliokithiri, usimamizi mbaya na umasikini nchini Guinea. Wanasema, hayo na mengine, ndiyo yaliyowasukuma kufanya mapinduzi.

Wanasema katiba imevunjwa na kwamba kutakuwa na mashauriano ya kuunda mpya serikali, inayowahusisha watu wote.

Wamedai pia kwamba serikali imevunjwa na kwamba mipaka ya ardhi itafungwa kwa wiki moja.

Katika picha na video zilizowekwa katika mitandao ya kijamii, mtu ambaye anaonekana kuwa rais Alpha Condé, amevaa mavazi ya kawaida na shati iliyochapishwa maua anaonyeshwa akiwa amekasirika, huku akiwa amezungukwa na wanaume walio na sare za jeshi.

Katika video moja, ameulizwa kwa Kifaransa ikiwa ameumizwa kwa njia yoyote, lakini rais huyo hakujibu lolote.

Ubalozi wa Australia umewahimiza raia wake kukaa mahali salama na kutazama vyombo vya habari vya ndani na taarifa kutoka kwa balozi.

Kumekuwa na ripoti nyingi za milio ya risasi katika mji mkuu wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi, jana Jumapili asubuhi.

Wakazi wa eneo hilo wameambia mashirika ya habari kuwa wanajeshi wamekuwa wakifanya doria mitaani na wamefunga daraja kuelekea mtaa ambao Ikulu ya rais ipo.

Wakazi wenye hofu ya wilaya kuu ya Kaloum wametii maagizo yao ya kukaa nyumbani.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kwamba daraja la pekee linalounganisha bara na eneo la Kaloum, ambalo lina wizara nyingi na Ikulu ya Rais, limefungwa na wanajeshi; wengine wakiwa na silaha nzito, walikuwa wamewekwa kuzunguka Ikulu.

Video zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha misafara ya magari ya kubeba silaha na malori yanayobeba askari wanaofanya doria mitaani, ingawa hizi hazijathibitishwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!