Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yatambulisha mpango maalum kuwahudumia walimu
Habari Mchanganyiko

NMB yatambulisha mpango maalum kuwahudumia walimu

Spread the love

KWA kutambua umuhimu wa walimu nchini na mchango wao katika mafanikio ya Benki ya NMB, taasisi hiyo kubwa kuliko zote za fedha nchini imeanzisha mpango maalum wa kuihudumia kada hii nyeti katika ujenzi wa taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

 

Utaratibu huo bunifu wa “Mwalimu Spesho – Umetufunza Tunakutunza” umetangazwa rasmi jana huko Songea mkoani Ruvuma wakati wa kongamano la walimu lililoandaliwa na benki hiyo.

 

Akiitambulisha programmu hiyo, Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi, Aikansia Muro, alisema Mwalimu Spesho ni suluhisho inayojumuisha huduma zote za kumwezesha mwalimu zinazotolewa na NMB kupitia fursa mbalimabli.

 

“Leo tumekuja na mpango maalum kwaajili ya walimu wetu. Mpango huu tuliouita ‘Mwalimu Spesho’ umejumuisha huduma zote zinazomuwezesha mwalimu,” afisa huyo aliwaambia washiriki wa kongamano hilo.

 

Huduma hizo ni pamoja na mikopo yenye riba nafuu, ikiwemo ya walimu kujiendeleza kielimu na kuwasomesha watoto wao, mikopo ya biashara ndogondogo, ujenzi, vyombo vya moto kama bodaboda na pikipiki za miguu mitatu.

 

Walimu pia watapata mkopo wa bima yaani Insurance Premium Finance (IPF), ambayo inawezesha kulipa bima kujikinga na majanga mbalimbali. Ipo pia mikopo ya pembejeo na mashine za kilimo; fursa za kushiriki promosheni na kujishindia zawadi mbalimbali pamoja na kupata elimu ya kifedha na faida nyingine lukuki.

 

Bi Muro alisema kongamano hilo ni siku maalum ya NMB kukutana na kuzungumza na walimu huku ikiwapa elimu ya fedha na kupokea kutoka kwao mrejesho na mawazo kuhusu huduma zake na jinsi ya kuziboresha. Pia ni wakati wa kuwajulisha walimu juu ya maendeleo ya taasisi hiyo pamoja na fursa mbalimbali zilizopo kwa ajili yao.

 

“Tunaamini, walimu hawa zaidi ya 200, watasaidia kupeleka elimu watakayoipata hapa kwa wenzao na hata familia zao na jamii kwa ujumla juu ya huduma nzuri zinazotolewa na Benki ya NMB,” alisisitiza.

 

Aidha alisema kuwa kutokana takribani Watanzania milioni 20 kutokuwa na akaunti za benki huku wengi wao wakimiliki simu zinazoweza kufanikisha miamala ya fedha, NMB imetumia maendeleo ya teknolojia za kidijitali kuwaingiza wananchi zaidi kwenye mifumo rasmi ya kifedha na kuipatia serikali mapato.

 

“Kupitia masuluhisho haya, Benki ya NMB imeweza kufikisha asimilia 94 ya miamala yake kupitia simu za mkononi,” Bi Muro alibainisha na kuongeza kuwa hivi karibuni wamezindua huduma kubwa tatu, ambazo zinaendelea kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya kibenki nchini.

 

“Huduma hizi ni mikopo ya kidijitali (MshikoFasta), NMB Pesa Wakala na NMB Lipa Mkononi. Kupitia mifumo hii tunaweza kuwafikia watanzania wengi zaidi na hivyo kuchangia kuongeza idadi ya watanzania wanaotumia huduma za kibenki na pia hata kuwasaidia walimu ambao wanaweza wakawa mbali na matawi ya benki. Ndiyo maana tunasema ‘Mwalimu Spesho- Umetufunza Tunakutunza’.”

 

Mgeni rasmi kwenye shughuli hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Labani Thomas, alisema NMB ni benki ya kuigwa linapokuja swala la kuwajali walimu na kulihudumia taifa akitolea mfano wa utaratibu wa Mwalumu Spesho ambao alisema ni fursa ya kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma za kifedha na kibenki.

 

Kanali Labani aliiambia hadhira hiyo kuwa jitihada za NMB zinaunga mkono juhudi za serikali za kuwajumuisha Watanzania wengi kitika mfumo rasmi wa kifedha ili kuinua vipato vyao na uchumi wa nchi kwa ujumla.

 

“Kwa upande wa bidhaa za akiba na mikopo, NMB ni miongoni mwa benki zinazoongoza kwa kubuni bidhaa zinazolenga mahitaji ya kila makundi ya wateja wake katika soko kama nyie waalimu na jamii kwa ujumla. Tarifa nilizo nazo ni kwamba NMB ni benki pekee ambayo imetoa mikopo mingi kwa wafanyakazi wa serikali kuu na serikali za mitaa ambapo asilimia kubwa ya walimu hapa nchini wamefaidika sana na mikopo hii,” kiongozi huyo alisema.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!