February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ndugai amtisha Heche Tarime Vijijini

Spread the love

JOB Nduga, Spika wa Bunge la Jamhuri amemtisha John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini kwamba, uchaguzi mkuu ujao jimbo hilo litarudi CCM mapema. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Ndugai amesema, kuna ufujaji mkubwa wa miradi ya serikali licha ya mbunge wake kuwa mpinzani na mpiga kelele.

Ameeleza kushangazwa na Heche kwa kushindwa kusimamia miradi ya Sh. 9 Bilioni iliyopo jimboni kwake.

“Ni lazima wabunge tujue miradi iliyo kwenye majimbo yetu,” amesema Ndugai na kuongeza;

“Sasa kama mtu kashindwa kusimamia miradi ya Sh. 9 Bilioni, mwakani atasema nini?”

Ndugai ametoa kauli hiyo leo tarehe 4 Februari 2019 bungeni Dodoma na kudai kwenye uchaguzi mkuu ujao katika jimbo hilo, wimbo utakuwa ni Sh. 9 Bilioni.

Ndugai amedai, kutokana na kushindwa kwa Heche kusimamia, ushindi kwa CCM utakuwa mapema.

error: Content is protected !!