March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Nape  Nnauye ajiuzulu

Spread the love

NAPE Nnauye, amejiuzulu uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili na Utalii. Kujiuzulu kwake, kunatokana kile kinachoitwa, “kugoma kunyofoa baadhi ya taarifa kwenye ripiti ya kamati yake.” Anaripoti Mwandishi Wetu kutoka Dodoma … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii zinasema, Nape amejiuzulu baada ya kushinikizwa na baadhi ya wakubwa ndani ya chama chake.

“Ni kweli kwamba Nape amejiuzulu. Ni baada ya kutaka ripoti ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii, iliombe Bunge kuundwa kwa Kamati Teule, ili kuchunguza utaratibu uliotumika wa kufuta mashamba ya baadhi ya wananchi,” ameeleza mjumbe mmoja wa kamati hiyo.

Ameongeza, “lakini serikali haitaki kuundwa kwa Kamati hiyo. Hivyo imeamua kutumia Kamati ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumlazimisha kujiuzulu.”

Taarifa zinasema, tayari Nape amemuandikia barua Spika ya kumjulisha kujiuzulu. Katibu wa Bunge, Steven Kigaigai, amemthibitishia mwandishi wa habari hii kujiuzulu kwa mwanasiasa huyo.

Machi mwaka juzi, Nape aling’olewa kwenye nafasi ya uwaziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo.

Mbunge huyo wa Mtama mkoani Lindi, alivuliwa wazifa wake huo, siku moja baada ya kupokea ripoti ya Kamati ya uchunguzi wa tukio la uvamizi wa kituo cha televisheni cha Clouds. Kituo hicho kilivamiwa na watu wenye silaha, wakiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Nape aliwahi kuwa Katibu wa Idara ya Uenezi ya CCM.

error: Content is protected !!