Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Tangulizi Kesi ya uchochezi; Mahakama yamtaka mdhamini wa Lissu
Tangulizi

Kesi ya uchochezi; Mahakama yamtaka mdhamini wa Lissu

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

HAKIMU Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba ameagiza wadhamini wa Tundu Lissu katika kesi inayohusu tuhuma za uchochezi kupitia gazeti la MAWIO, wafike mbele yake na kueleza sababu za kutofika kwake mahakamani. Anaripoti Faki Sosi… (endelea)

Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu Mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ni mtuhumiwa wa nne katika kesi ya jinai namba 204 ya mwaka 2016.

 Wadhamini wa Lissu wanaohitajika mahakamani ni Robert Katula na Ibrahim Ahmed.

Mtuhumiwa Lissu amekuwa nje ya nchi kwa muda mrefu kwa ajili ya matibabu ya kiwango cha juu kitaalamu baada ya kutoka hospitali ya jijini Nairobi, Kenya ambako alikimbizwa baada ya kupata matibabu ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Lissu alipelekwa hospitali baada ya kushambuliwa kwa risasi kadhaa akiwa ndani ya gari wakati akiwasili eneo la Area D mjini Dodoma akitokea bungeni.

Tukio hilo la Septemba 7 mwaka 2017, lililotokea siku chache baada ya mwenyewe kutangaza mbele ya vyombo vya habari kuwepo “vijana wa usalama” wanaomfuatilia kwa gari kila aendeko. Alitaka wakuu wa Idara ya Usalama na yombo vingine vya ulinzi vya serikali waagize vijana wao kuacha kumfuatilia kwa sababu “mimi si jambazi.”

Tangu aliposhambuliwa katika tukio analolitaja binafsi kuwa ni jaribio la kumuua, Lissu amekuwa hatokei mahakamani kwa sababu anaendelea na matibabu nje ya nchi.

Baada ya hospitali ya Nairobi ambako alikamilisha sehemu ya matibabu maalum, Lissu alipelekwa nchini Ubelgiji na hivi karibuni amejitokeza hadharani akisema amekamilisha sehemu ya tiba na sasa ameanza awamu ya kufanya mazoezi ya kutembea bila ya magongo.

Lissu ameumia zaidi miguu ambamo anasema amefanyiwa operesheni 20 zilizofanikisha kumuweka bila ya jeraha na aina yoyote ya chuma mwilini.

Huku kukiwa na taarifa za kutakiwa arudi nchini kama alivosikika Spika Job Ndugai aliyemtishia.

“kumtoa nje ya uwanja,” mwenyewe amesema atarudi siku inayofuata kutoka pale atakapopewa taarifa na daktari wake nchini Ubelgiji kuwa amekamilisha tiba yake.

Kwa sasa anaonekana akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mkasa uliomfika na masikitiko yake kuwa hakuna mtu aliyekamatwa wala uchunguzi unaofanyika.

Lissu anaituhumu serikali kuwa inawajua waliokusudia kumuua kwa kuyatazama mazingira ya kutokea kwa tukio hilo.

Kauli ya mwisho ya Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro ni kwamba uchunguzi unaendelea.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema: Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!