December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wananchi walazimishwa kuchukua fedha zao

Spread the love

SERIKALI imetoa wiki moja kwa wananchi wa Nyamongo mkoani Mara waliohamishiwa makazi yao kwa ajili ya kupisha shughuli za uchimbaji madini katika mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya Madini ya Acacia, kuchukua fedha zao za fidia. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea.)

Agizo hilo limetolewa leo tarehe 5 Februari 2019 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo wakati akijibu swali la Mbunge wa Bunda, Mwita Getere aliyesema tatizo la fidia kwa wananchi wa Nyamongo limekuwa la muda mrefu, na kuihoji serikali lini itahakikisha wananchi hao wanalipwa fidia zao.

Akijibu swali hilo, Nyongo amesema kuna wananchi takribani 138 waliofanyiwa uhakiki na fedha zao kutoka, wamesusa kuchukua fedha hizo kwa madai kuwa ni ndogo, ambapo amewataka wananchi hao kuacha kususa fedha hizo, na kwamba wasipozichukua serikali ya mkoa itafanya vinginevyo.

“…Wananchi 138 wamefanyiwa uhakiki  na kuna cheki ya bilioni 3.2 wamegoma kuchukua sababu ya kulishana maneno, wananchi ambao cheki zao ziko tayari wakachukue ndani ya wiki hii, wasipochukua serikali ya mkoa itafanya vinginevyo, North Mara tumeshawaambia ndani ya wiki hii maeneo ambayo hayana tatizo walipe mara moja,” ameagiza Nyongo.

Aidha, Nyongo ameeleza sababu mbili zilizopelekea wakazi wa Nyamongo kuchelewa kulipwa stahiki zao, ikiwemo baadhi yao kufanya udanganyifu kwa kuongeza mazao na kujenga majengo baada ya maeneo yao kufanyiwa uhakiki na kupelekea thamani iliyopatikana katika uhakiki wa kwanza kuwa kubwa tofauti na uhalisia.

“Madai ya Nyamongo yamechukua muda mrefu, kuna sababu mbili sababu ya kwanza Acacia kuchelewa kufanya malipo kwa muda stahiki, ya pili ni ya wananchi wenyewe, waliongeza majengo waliongeza mazao inatupa shida sana sababu ‘evaluation’ ya kwanza inaonekana ndogo ya pili inaonyesha kubwa, hili limefanya kampuni kushindwa kulipa.

Hili suala lipo kwa chief value na liko ktk evaluation na evaluation itakayotolewa kampuni ilipe mara moja, tumekubaliana mgodi wa North Mara na Acacia walipe mara moja wananchi,” amesema Nyongo.

error: Content is protected !!