Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Biashara NBC yazindua kampeni ya kumwaga zawadi msimu wa sikukuu
Biashara

NBC yazindua kampeni ya kumwaga zawadi msimu wa sikukuu

Spread the love

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua kampeni yake ya msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka  inayofahamika kama “Tabasamu Tukupe Mashavu,” ikilenga kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu, vocha za manunuzi na punguzo la bei kwenye huduma mbalimbali za kijamii na manunuzi ya vifaa vya kielektroniki.

Kwa kampeni hiyo inalenga kutoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kufurahia pamoja na wapendwa wao wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mkurugenzi wa Idara ya Wateja wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC, Elibariki Masuke (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni ya msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka inayofahamika kama “Tabasamu Tukupe Mashavu.” Wengine ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Biashara ya simu Tanzania kampuni ya Samsung, Mgope Kiwanga, Mkuu wa Idara huduma za benki Kidigitali NBC, Ulrik Peter (wa pili kushoto) na Meneja Masoko na Uhusiano wa Migahawa ya Samaki Samaki, Azmina Mohamed (kushoto).

Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo ilifanyika mapema leo Jumatano makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo kampuni washirika wa kampeni hiyo kama Samsung, Auto Express, AG Energies, PUMA, Samaki Samaki, ABC Emperio na wafanyakazi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo na Wakubwa wa benki hiyo, Elibariki Masuke.

“Jina la kampeni, “Tabasamu Tukupe Mashavu,” linakwenda sambamba na kiini cha msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka, ambapo “Tabasamu” inaashiria furaha inayotokana na uwezo wa kufanya miamala na malipo popote ulipo huku “Mashavu” ni pale unapopata huduma nzuri na za kuridhisha tena kwa kurudishiwa thamani zaidi.

“Kimsingi kampeni hii imebuniwa ili kuwahamasisha wateja wetu kushiriki furaha ya miamala na marafiki, familia, na wapendwa wao katika kipindi hiki cha sikukuu, wakiwa na uhakikisho kwamba NBC iko tayari kuwaunga mkono kwa kutoa zawadi za kuvutia,” Ameeleza Masuke.

Mkurugenzi wa Idara ya Wateja wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC, Elibariki Masuke (wa pili kushoto) sambamba wawakilishi wa kampuni wadau wa benki hiyo, Mkuu wa Idara ya Biashara ya simu Tanzania kampuni ya Samsung, Mgope Kiwanga (wa pili kulia), Mkuu wa Idara huduma za benki Kidigitali NBC, Ulrik Peter (kulia) na Mkuu wa Idara ya wateja wakubwa na wadogo wa kampuni ya AutoExpress, Erick Munene (kushoto) wakionyesha baadhi ya zawadi zinazousishwa kwenye ya msimu wa Sikukuu za mwisho wa mwaka inayofahamika kama “Tabasamu Tukupe Mashavu.”

Kwa mujibu wa Masuke katika kipindi chote cha kampeni hiyo ya mwezi mmoja, wateja wa benki hiyo watakuwa kwenye nafasi kufurahia upendeleo wenye kuvutia kwenye maeneo mbalimbali kama vile maduka, supermarkets na mtandaoni.

“Zaidi wateja wetu watakuwa kwenye nafasi zawadi mbalimbali kama vile smart TV ZA Samsung, simu janja za Samsung Galaxy Z-Flip 4, na Vocha za kufanya manunuzi zenye thamani ya hadi Tsh 500,000.

“Pia mawaka wetu na wateja wetu wenye mashine za malipo ya NBC (POS) wanazi nafasi za kujishindia pesa taslimu,’’ amesema.

Amesema ili kushiriki kwenye kampeni hiyo wateja wa benki hiyo wanatakiwa kutumia kadi zao za NBC VISA kufanya miamala kwenye mashine za ATM, Wakala, maduka, vituo vya mafuta, baa, migahawa, Airbnb, safari, hoteli na malipo mbalimbali ya mtandaoni kama vile Netflix, Amazon, na usajili wa mtandaoni.

“Tunataka kugeuza kila shughuli kuwa sherehe msimu huu wa sikukuu kupitia kampeni hii ya ‘Tabasamu Tukupe Mashavu’. Kutumia kadi yako ya NBC VISA kunafungua milango ya ulimwengu wa zawadi.

Mkuu wa Idara ya Biashara ya simu Tanzania kampuni ya Samsung, Mgope Kiwanga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni ya msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka inayofahamika kama “Tabasamu Tukupe Mashavu.” Wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Wateja wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC, Elibariki Masuke (wa pili kushoto), Mkuu wa Idara huduma za benki Kidigitali NBC, Ulrik Peter (kushoto), Mkuu wa Idara ya wateja wakubwa na wadogo wa kampuni ya AutoExpress, Erick Munene (kulia) na Kiongozi wa timu ya Mauzo ya Kampuni ya AG Energies, Ester Golan (wa pili kulia)

“Iwe unafanya ununuzi, unakula, unajaza mafuta kwenye vituo vya mafuta, au kufurahia wakati wako huku ukiwa umekaa kwa utulivu katika Airbnb au hoteli, kila ‘unapochanja’ unazidi kujileta karibu na zawadi za kusisimua kama ikiwemo kurudishiwa pesa taslimu na mapunguzo ya bei kwenye huduma za washirika wetu,” ameongeza.

Masuke ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wateja wa benki hiyo kutumia huduma za NBC Kiganjani, ATM, na NBC Wakala kulipa kufanya miamala na kutuma fedha kwa wapendwa wao katika msimu huu wa sikukuu.

Kwa upande wao kampuni wadau wa kampeni hiyo wakiwemo Samsung, Auto Xpress, AG Energies, Samaki Samaki, na ABC Emperio wamesisitiza dhamira yao kupunguza bei kwenye bidhaa zao ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao kwenye kampeni hiyo lengo likiwa ni kutoa unafuu kwa wateja wa benki ya NBC kupata fursa ya kufurahia sherehe za mwisho wa mwaka sambamba na wapendwa wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

Biashara

Cheza kwa kuanzia Sh 400 kushinda mgao wa Expanse Tournament kasino 

Spread the love  UKISIKIA bosi kacheka ujue Maokoto yanafuatia, Kupitia promosheni pendwa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

error: Content is protected !!