Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Nathwani na Sangita mahakamani kwa kujeruhi jirani
Habari Mchanganyiko

Nathwani na Sangita mahakamani kwa kujeruhi jirani

Spread the love

KESI inayowakabili mkazi wa Dar es Salaam, Bharat Nathwani (57), maarufu kwa jina la Chiku na mke wake Sangita Bharat Nathwani (54) inatarajiwa kuanza kusikilizwa ushahidi Februarri 19 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, ambako wakituhumiwa kwa mashitaka manne likiwemo la kujeruhi na kutoa lugha ya matusi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Wanandoa hao ambao ni raia wa Tanzania wenye asili ya India wanaoishi Mrima – Kisutu kwenye jengo la Lohana, Dar es Salaam walifikishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya wa mahakama hiyo na kusomewa mashitaka yao na wakili wa serikali.

Katika hati ya mashitaka, washitakiwa hao wanaotuhumiwa kwa mashitaka manne, ambayo wanadaiwa kuyatenda Julai 21,2023 ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Katika shitaka la kwanza la kujeruhi linalomkabili Nathwani (Chiku) peke yake, anatuhumiwa kuwa Julai 21,2023 akiwa eneo la Mrima-Kisutu, jengo la Lohana ndani ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam alimjeruhi jirani yake.

Nathwani anadaiwa kumsababishia madhara makubwa mke wa jirani yake, Kiran Lalit kwa kuzamisha kichwa chake kwenye ndoo ya saruji na kumjeruhi katika macho na sikio na kwa kumpiga katika shingo na kumsababishia maumivu.

Pia, katika shitaka la pili la shambulio la mwili linalomkabili Nathwani (Chiku) peke yake, tarehe hiyo na eneo hilo alimsababishia madhara kwa kumshambulia jirani yake Lalit Ratilal katika mwili wake kwa kumpiga ngumi na mateke kichwani.

Ilidaiwa kuwa katika shitaka la tatu na la nne linalomkabili mke wake Sangita peke yake, ambapo anatuhumiwa kutoa matusi makubwa dhidi ya majirani zake, Lalit na Kiran  kitendo ambacho kilileta fujo kwa namna ambayo inaweza kuleta uvunjifu wa amani.

Kesi hiyo ilitakiwa kuanza kusikilizwa Jumanne  mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Aaron Lyamuya, lakini ilishindikana kwa sababu hakimu huyo hakuwepo mahakamani kutokana na majukumu mengine aliyokuwa nayo.

Wakili wa Serikali, Frank Michael alidai juzi  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga wa mahakama hiyo kuwa kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa na pia wana mashahidi wawili na wako tayari kuendelea.

“Mheshimiwa tunao mashahidi wawili na tupo tayari kuendelea, lakini tulikuwa tunaomba tarehe nyingine ya usikilizwaji kwa sababu hakimu anayesikiliza kesi hii hayupo,” alidai Wakili Michael.

Hakimu Kiswaga aliwataka mashahidi hao kufika mahakamani hapo Februari 19,2024 kwa ajili ya kutoa ushahidi wao.

” Mashahidi nawataka mfike tarehe hiyo na huyo shahidi ambaye amesema  tarehe hiyo hatakuwepo atawasiliana na wakili wa serikali atatoa ushahidi wake kwa njia ya mtandao ‘Video Conference’ kwa sababu vifaa vipo,” alidai

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

error: Content is protected !!