Tuesday , 14 May 2024
Home Kitengo Biashara NMB yazindua mchakato wa “NMB Pesa Haachwi Mtu”
Biashara

NMB yazindua mchakato wa “NMB Pesa Haachwi Mtu”

Spread the love

BENKI ya NMB imeanzisha kampeni kubwa ya kuhamasisha na kuwawezesha watu wengi kufungua akaunti ili waweze kunufaika na faida za kuwa sehemu ya mfumo rasmi wa fedha. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Kampeni hiyo inayoitwa “NMB Pesa Haachwi Mtu” ilitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa benki hiyo, Filbert Mponzi, wakati wa kipindi cha Joto la Asubuhi cha Redio ya EFM.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto), akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wananchi kufungua akaunti ya NMB Pesa kwa Sh 1,000 tu katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni watangazaji wa E-FM, Mussa George na Emmanuel Mgaya ‘Masanja’.

Kiongozi huyo alisema lengo kuu la mchakato huo kupitia huduma ya NMB Pesa Akaunti ni kusaidia kuongeza idadi ya watu wenye akaunti za benki nchini na wale wanaohudumiwa na taasisi hiyo ambao sasa hivi ni zaidi ya milioni sita.

“Utafiti wa Finscope wa hivi karibuni unaonyesha kwamba kwa sasa ni watu asilimia 22 tu kati ya wale wenye sifa za kuwa na akaunti za benki nchini ndio wanazo, kiasi ambacho ni kidogo sana,” Mponzi alibainisha kwenye kipindi hicho kilichorushwa moja kwa moja kutoka makao makuu ya benki hiyo.

Akifafanua, alisema NMB kama benki kinara nchini inawajibu wa kusaidia kutatua changamoto hiyo ndiyo maana ukafanyika uamuzi wa kuendesha kampeni hiyo inayowalenga hasa wananchi wa kawaida hususani mama ntilie, wamachinga na waendesha boda boda.

Katika kufanikisha zoezi hilo, Mponzi alisema akaunti ya NMB Pesa inafunguliwa kwa Sh 1,000 tu na aina makato ya kila mwezi.

Alisema lengo la unafuu huo ni kuondoa ile dhana ya kuwa kufungua akaunti ni jambo aghali linalohitaji fedha nyingi.

“Ufunguaji NMB Pesa Akaunti utafanyika kirahisi sana mahala popote kidijitali na maafisa mauzo wetu ambao ni maalumu kwa ajili ya kazi hiyo,” Mponzi alibainisha.

“Kupitia mchakato huu, tunataka kutimiza ndoto za wale wote wanaohitaji kuwa na akaunti za benki,” aliongeza na kusisitiza kuwa NMB Pesa Akaunti ina faidi lukuki.

Faida hizo ni pamoja na kuunganishwa na huduma ya NMB Mkononi ambayo faida zake nyingi ni pamoja na mikopo ya Mshiko Fasta isiyokuwa na dhamana inayoaanzia Sh 1,000 hadi Sh 500,000.

Akaunti hii pia inakuwa na huduma ya bima ya TZS 200 kwa mwezi ambayo ina mkono wa kwa heri wa TZS milioni 2 ikitokea mwenye akaunti akafa au akapata ulemavu wa kudumu au akafiwa na mwenza wake.

Akizungumza baada ya kurushwa kwa kipindi hicho, Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Matawi na Mauzo wa NMB, Bw Donatus Richard, aliwahasa wananchi kuitumia fursa ya NMB Pesa Akaunti kunufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.

Alisema hili kukidhi mahitaji ya soko, wataendelea kuja na bidhaa na huduma bunifu zitakazosaidia kutatua changamoto za kifedha za wananchi kama sehemu ya kuendeleza ajenda ya huduma jumuishi za kifedha nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaitambulisha rasmi ‘NBC Connect’ Zanzibar

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetambulisha rasmi huduma yake...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya kidijitali kwa wajasiriamali

Spread the loveBENKI ya NMB imezindua akaunti maalum ya kidijitali iitwayo ‘NMB...

Biashara

EXIM Bank, Msalaba Mwekundu wapanda miti, wachangisha damu

Spread the love  BENKI ya Exim imeshirikiana na Chama cha Msalaba Mwekundu...

Biashara

Maokoto yameongezeka leo kwenye Expanse Tournament kasino

Spread the love  Maokoto yameongezeka kwenye promosheni ya Expanse inayoendelea kutimua vumbi...

error: Content is protected !!